Featured Kitaifa

”TUWE NA USHIRIKA IMARA WENYE KUKUZA UCHUMI’-DKT CHUACHUA

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua ,akizungumza wakati akifunga Kongamano la ushirika kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Na Alex Sonna-TABORA

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Dkt. Rashid Chuachua, amewaasa wanaushirika kutumia Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kujitafakari na kuangalia Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu ili kutumia Ushirika kwenye kukuza uchumi wa nchi.

Dkt.Chuachua ametoa kauli hiyo Juni 30, 2023 mjini Tabora kwenye Kongamano la Wanaushirika lililokuwa na lengo la kujadili maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho na kuishauri Serikali.

Amesema ni muhimu maadhimisho hayo yakatumika kuangalia maeneo hayo ili kujiimarisha na kujiletea maendeleo endelevu ya ushirika nchini.

“Nikupongeze Mrajis kwa kazi unayofanya ya kusimamia Ushirika nchini, dhamira ya Serikali ni kuona Ushirika unakuwa na maendeleo endelevu katika shughuli za uchumi na jamii yanafikiwa, hii ni sekta mtambuka yenye kusimamia uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi wa mwanachama mmoja mmoja,” amesema.

Aidha, amesema maadhimisho hayo yanatoa dira na mwelekeo wa kuisaidia Wizara kutatua changamoto zilizopo leo ili kesho zisiwepo tena na kwamba maadhimisho hayo lazima yatoe matokeo yanayopimika ili kuona manufaa yake.

Kadhalika, amesema kuna tatizo la weledi wa taaluma ya hesabu kwa watumishi wa vyama vya ushirika na kupongeza Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kwa kazi kubwa waliyofanya ya kuwa na mafunzo mbalimbali yanayotolewa bila kuzingatia viwango vya elimu ili kuwa na ufanisi kwenye hesabu za ushirika.

Awali, amesema wanaushirika wamejengewa uwezo kupitia makongamano mbalimbali ikiwamo masuala ya kodi, elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa, masoko ya bidhaa na huduma na ukaguzi katika vyama vya ushirika kufikia maendeleo endelevu.

“Mmeshiriki kongamano la biashara na uwekezaji kwa vyama vya ushirika kutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na Nafasi ya Ushirika kuanzisha viwanda vidogo vidogo pamoja na fursa ya uwekezaji katika hisa za benki, vipande na soko la mitaji kukuza fursa za uwekezaji, pia kongamano la Sekta ya Huduma za Fedha na TEHAMA ikiwa na uzoefu katika huduma za kifedha za benki na SACCOS pamoja na Ushirika kujiendesha kidigitali ikiwa ni pamoja na matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa vyama vya ushirika ili kuleta maendeleo endelevu,” amesema.

Naye, Mrajis wa Vyama Vya Ushirika na Mtemdaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amesema Tume hiyo inaendelea kutekeleza ipasavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika eneo la Ushirika kutokana na kuwekewa msisitizo kwa kutajwa mara 85.

“Kongamano hili limetokana na majukwaa ya Ushirika kwenye mikoa, kuna suala la vyama vingi vya Ushirika wa mazao kwa mfano Tumbaku tuna vyama vya kilimo lakini baada ya mauzo wananchi hawapati namna ya kutunza fedha zao kwa mwisho wa siku fedha zinaisha na inapofika mwisho wa msimu wanarudi kwenye utumwa wa kukopa, hapa wameongea kuhusu Benki ya Ushirika na kuweka mikakati, kuhusu Stakabadhi za Ghala, sera na sheria ya Ushirika na Ushirika kufanya kazi kibiashara,” amesema.

 Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua ,akizungumza wakati akifunga Kongamano la ushirika kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akielezea malengo ya Kongamano la ushirika kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe.Onesmo Buswelu,akizungumza wakati wa Kongamano la ushirika kuelekea  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Moshi (MoCU) Prof.Alfred Sife,akizungumza wakati wa Kongamano la ushirika kuelekea  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Katibu Mtendaji wa Shirika la Vyama vya Ushirika (TFC) Bw.Alex Ndikilo,akitambulisha Meza Kuu wakati wa Kongamano la ushirika kuelekea  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Ndg Majaliwa Bilali,akizungumza wakati wa Kongamano la ushirika kuelekea  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua (hayupo pichani) wakati akifunga Kongamano la ushirika kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua,akikabidhi tuzo mbalimbali kwa taasisi zilizosaidia kuandaa Maandalizi ya  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga  Kongamano la ushirika kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua,akizindua Tovuti (Website) ya mfuko wa tafiti za ushirika katika kuelekea  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua  Dkt Rashid Chuachua,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Tafiti za Ushirika mara baada ya kuzindua Tovuti (Website) ya mfuko wa tafiti za ushirika katika kuelekea  Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani yatakayofanyika kesho Julai Mosi  mwaka huu katika Viwanja vya Ipuli  Mkoani Tabora.

About the author

mzalendoeditor