Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI MWANAID AFUNGUA MAFUNZO YA SAYANSI YA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto,Sebastian Kitiku,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Mratibu Mradi wa Watoto wetu Mkoa wa Dodoma ambaye alimwakilishi Mkurugenzi wa Children in Cross Fire,Bw. Frank Samson,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Makuzi ya Mtoto Tanzania TECDEN Mwajuma Rwebangila ,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo ya Sayansi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika leo Juni 26,2023 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna, DODOMA.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum, Mwanahidi Ally Khamisi amefungua mafunzo ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa wataalam ngazi ya Taifa na Mikoa huku akiwataka wataalamu hao kutumia elimu hiyo kwenye maeneo yao ya kazi .

Akizungumza leo June 26,23 Jijini Dodoma,Naibu Waziri huyo amesema Wataalamu wàliopo katika mafunzo hayo ni muhimu katika malezi na makuzi ya watoto hivyo ni matarajio kuwa litakochochea utekelezaji mkubwa zaidi kwenye program ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Watoto.

Amesema,Mafunzo ya wakati hayo yamekuwa na upekee kwa kuwa yanajumuisha washiriki wengi zaidi, kwa idadi ya jumla ya washiriki 134 kutoka Mikoa 16 na hivyo kuwa na Matumaini ya kuifikia mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

“Niwashukuru sana waandaji wote kwa jitihada hizi, naamini baada ya Mafunzo haya tunatarajia kuwepo na watendaji wengi zaidi katika ngazi mbalimbali na hivyo kuwa na uhakika kuwa programu hii inaratibiwa na kusimawiwa na watu sahihi wenye uelewa kuhusu malezi na makuzi ya watoto,”amesema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Makuzi ya Mtoto Tanzania TECDEN Mwajuma Rwebangila ni kati ya kundi lililoingia mkataba nchi nzima kwa kuwezesha maboresho ya malezi ya mtoto na kuongeza utaalamu kwa wataalamu kitaifa kwa kufanya mafunzo kikamilifu kutoka kwa watoto asilimia 26 hadi kufikia asilimia 53 kwa utimilifu wa akili.

Aidha ameeleza kuwa mtandao huo umekuwa ukihamasisha zaidi jamii kujua umuhimu wa kuwepo kwa uboreshaji wa marezi na makuzi kwa watoto kwa lengo la kupata watoto wenye timilifu wa akili kwa lengo lakuwa na taifa bora na lenye kuwa na wazalishaji wenye tija badala ya kuwa na jamii kubwa yenye kuwa na wazalishai wachache.

Naye Mwakilishi w chuo kikuu cha Aghakani kutoka nchini Kenya Prof. Amina Abubakari amesema kuwa yeye akiwa mwadhili kutoka chuo hicho anayo amani kubwa ya kushirikiana na wataalamu wa kulinda maendeleo ya watoto nchini Tanzania jambo ambalo alisema kuwa ni njia pekee ya kuwezesha kizazi cha umri huo kuwa imara katika utimilifu wa akili lakini pia jamii kutambua umuhimu wa kulinda na kuzingatia malezi ya mtoto .

“Tunatakiwa kuwapatia mafunzo watoto wetu wenye umri kuanzia siku 0 hadi kufikia miaka 8 kwa lengo la kuwa na kzazi imara na chenye uwezo mkubwa wa kufikiri kwa mapana jambo ambalo ameeleza kuwa linaweza kusababisha kuwepo kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi jambo ambalo linafanya kuwepo kwa uhakika wa kuwa na watu wa taifa sahihi zaidi” alisema Prof.Amima.

Akifungua mafunzo hayo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum, Mwanahidi Ally Khamisi akifungua mafunzo hayo ya Siku tano ambayo yanawahusisha Mafisa maendeleo ya Jamii wa Mkoa na Taifa pamoja na wadau mbalimbali, alisema kuwa mafunzo hayo yanataka kufanywa kwa uaminifu mkubwa na uadilifu ili kuhakikisha elimu hiyo inapelekwa kwa ngazi zote.Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Makuzi ya Mtoto Tanzania TECDEN Mwajuma Rwebangila ni kati ya kundi lililoingia mkataba nchi nzima kwa kuwezesha maboresho ya malezi ya mtoto na kuongeza utaalamu kwa wataalamu kitaifa kwa kufanya mafunzo kikamilifu kutoka kwa watoto asilimia 26 hadi kufikia asilimia 53 kwa utimilifu wa akili.

Aidha ameeleza kuwa mtandao huo umekuwa ukihamasisha zaidi jamii kujua umuhimu wa kuwepo kwa uboreshaji wa marezi na makuzi kwa watoto kwa lengo la kupata watoto wenye timilifu wa akili kwa lengo lakuwa na taifa bora na lenye kuwa na wazalishaji wenye tija badala ya kuwa na jamii kubwa yenye kuwa na wazalishai wachache.

Naye Mwakilishi w chuo kikuu cha Aghakani kutoka nchini Kenya Prof. Amina Abubakari amesema kuwa yeye akiwa mwadhili kutoka chuo hicho anayo amani kubwa ya kushirikiana na wataalamu wa kulinda maendeleo ya watoto nchini Tanzania jambo ambalo alisema kuwa ni njia pekee ya kuwezesha kizazi cha umri huo kuwa imara katika utimilifu wa akili lakini pia jamii kutambua umuhimu wa kulinda na kuzingatia malezi ya mtoto .

“Tunatakiwa kuwapatia mafunzo watoto wetu wenye umri kuanzia siku 0 hadi kufikia miaka 8 kwa lengo la kuwa na kzazi imara na chenye uwezo mkubwa wa kufikiri kwa mapana jambo ambalo ameeleza kuwa linaweza kusababisha kuwepo kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi jambo ambalo linafanya kuwepo kwa uhakika wa kuwa na watu wa taifa sahihi zaidi” alisema Prof.Amima.

About the author

mzalendoeditor