Featured Kitaifa

TUFANYE KILIMO RAFIKI ” WATAALAMU SUA”

Written by mzalendoeditor
Katika kukabilina na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba nchi na Dunia kwa ujumla, watanzania wametakiwa kufanya kilimo, uvuvi na ufugaji rafiki na mazingira, kwani tafiti zinaonyesha kwa kiasi kikubwa maeneo ya vyanzo vya maji yameathiliwa na shughuli za kibinadamu.
Mratibu wa Utafiti na Machapisho katika  Kurugenzi ya Shahada za Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaaluma kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Japhet Kashaigili kwenye kongamano la Kisayansi linalohusisha watafiti na wataaluma walio katika sekta mbalimbali.
Amesema tafiti zilizofanywa na wataalumu kutoka SUA zinaonyesha kilimo kisicho rafiki na mazingira, kuwepo kwa idadi kubwa ya mifugo kwenye eneo dogo na ukataji wa miti kiholela ni miongoni mwa  changamoto kubwa zinazochangia madiliko ya tabianchi. 
 “Matokeo ya tafiti yanaonesha kwamba tukiweza kufanya vizuri katika kurudisha uoto wa asili, tunaweza kupunguza  uzalishaji wa Tope kwenye mabwawa na kuongeza uwezo wa maji kuvivia chini ya udongo, na kutusaidia uwepo wa maji katika mito wakati wa kiangazi.” Alisema Prof. Kashaigili
 Pia amesema suala la kutumia maji chini ya ardhi halikwepeke hivyo kuna haja ya kutumia teknolojia kutambua kwa urahisi eneo gani lina maji, maji ya aina gani bila ya kuharibu mazingira kwa kuchimba ardhi ili kupata maji.
“Tukitumia vizuri Teknolojia itatusaidia kujua aina ya maji yaliyopo chini ya ardhi, tuchimbe umbali gani, pia inatupunguzia gharama maana unaweza kuchimba ukakuta hakuna maji.Alisema 
 “Hivyo utafiti unatuonyesha kwamba tukifanya vizuri katika Teknolojia  na kutumia tafiti kwa kuzitoa sehemu moja na kusambaza sehemu nyingine  tunaweza kuitambua hali ya maji chini ya ardhi” aliongeza.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda, amesema Serikali kupitia Chuo imekuwa kikitoa fedha kwa wataalamu kwaajili ya kufanya tafiti ili kupata suruhisho la changamoto  zinazoikumba nchi hasa katika  mabadiliko ya tabianchi, kilimo, misitu  na mifuo.
Mhadhili msaidizi, Idara ya Mimea, Vipando na Mazao ya Bustani, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Caroleni Maro ni miongoni mwa Wataalamu ambae amefanya utafiti kutambua ni namna gani watu wanaweza kuboresha vyakula vyenye virutubisho vya kukabilina  na matatizo ya afya na upungufu wa madini kwa watoto.
Amesema utafiti wake anaufanya kwenye mazao ya maharage katika maeneo ya nyanda za  kusini mwa Tanzania hasa mikoa ya Mbeya na Iringa na kwamba tafiti zinaonesha kwamba maharagwe yanavitamini C ya kutosha ukilinganishwa na ile iliyopo kwenye machungwa.
Amesema mbali na vitamin C pia yana madini chuma, vitamini A na kwamba kwa sasa wapo katika hatua ya kuangalia namna bora ya kuhifadhi majani hayo ili yaendelee kuwa ubora unatakiwa bila ya kupoteza vitamini pamoja na kuhimiza jamii ambazo zinalima maharagwe lakini hazitumii majani yake kama chakula kwa sababu mbalimbali.
Kongamano hilo la 18 la kisayansi  ni sehemu ya maadhimisho miaka  39 ya kumbukizi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine, ambapo kwa mwaka 2023 yatafanyika  siku nne mfululizo Mei 23 – 26 yakiambatana  na maonesho ya kitaaluma.

About the author

mzalendoeditor