Featured Michezo

YANGA SC BADO MOJA TU ITWAE TAJI LA 29 LIGI KUU TANZANIA BARA

Written by mzalendoeditor

MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Timu ya Yanga SC imekaribia kutwaa taji la 29 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji  Singida Big Star mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Liti Mjini  Singida.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa kupitia kwa Kiungo Mshambuliaji Stephane Aziz Ki pamoja na Mshambuliaji chipukizi Clement Mzize yote yakifungwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Yanga ilirudi ikiwa inahitaji mabao zaidi kwani ilikuwa inalisakama lango la mpinzani japokuwa hawakufanikiwa kuongeza mabao mengine mpaka dakika 90 mpira kumalizika matokeo yakiwa 2-0.

Kwa matokeo hayo Yanga SC wamefikisha Pointi 71 huku wakihitaji Pointi tatu waweze kutangazwa Mabingwa Msimu wa 2023/24 na kuwaacha watani zao Simba SC wakiwa na Pointi zao 64 timu zote zikiwa zimebakiwa mechi mitatu Ligi kumalizika.

About the author

mzalendoeditor