Featured Kitaifa

THE ROBI’S BAR & GRILL YAFUNGULIWA RASMI …”TUNAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUCHOCHEA MAENDELEO”

Written by mzalendoeditor
 
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Uwanja mpya wa Burudani maarufu The Robi’ s Bar & Grill umefunguliwa rasmi Mjini Shinyanga kwa ajili ya kutoa huduma za chakula na vinywaji.
 
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa The Robi’ s Bar & Grill leo Jumamosi Aprili 22,2023, wakati wa Sikukuu ya Eid El Fitr Mkurugenzi wa Baa ya The Robi’s Bar & Grill , Bi. Josephine Wambura amesema miongoni mwa sababu za kufungua baa hiyo ya kisasa iliyopo jirani na jengo la NSSF au Posta barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza ni kupanua huduma ya chakula na vinywaji pamoja na kutoa ajira kwa wananchi.
 
“Sisi ni wakazi wa Shinyanga na wawekezaji wazawa na tumeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya mkoa wa Shinyanga ili kuleta mabadiliko yenye matumaini ya kuchochea uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla”, amesema Bi. Josephine ambaye ni Mkurugenzi wa Karena Hotel, Level One Pub, Karena Annex Hotel.
 
“Tunawakaribisha wakazi wa Shinyanga na wageni mbalimbali wanaofika mkoani Shinyanga tuwahudumie kwani dhamira yetu ni kutoa huduma bora pamoja na ajira ili kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuchochea gurudumu la maendeleo”,ameeleza Bi. Josephine
 
Amesema The Robi’s Bar & Grill inapatikana ndani ya Karena Annex Hotel iliyopo jirani na NSSF barabara ya Shinyanga- Mwanza. Ndani ya Karena Annex Hotel pia kuna VIP Lounge. The Robi’s Bar & Grill ni sehemu ya Kampuni mama ya Karena Hotel Limited ambayo inatoa huduma ya malazi,chakula, kumbi za mikutano na sherehe mbalimbali.
“Karena Hotel Limited ambayo ni Kampuni tanzu pia ina kampuni ya Nancy Royal Food, ambapo ndani ya Nancy Royal Food kuna viwanja vya starehe ambavyo ni Canai Pub, Hennessy, VIP Lounge na Level One Pub ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za chakula, vinywaji na tunatoa huduma kwenye shughuli mbalimbali na hivi karibuni tutafungua Night Club ya Kisasa”,ameongeza.
 
Kupitia viwanja hivyo vya kisasa vya burudani pia kuna Screen kubwa kwa ajili ya kushuhudia michezo mbalimbali ili kuwapa burudani zaidi wateja.
 
Nancy Royal Food pia inatoa huduma za chakula na vinywaji hata nje ya Hoteli kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo harusi, mikutano, vikao, kipaimara,michezo, misiba n.k
 
 
Kwa Mawasiliano zaidi piga simu 0755923249 au 0756039449 au 0767811412
 
Muonekano wa sehemu ya The Robi’ s Bar & Grill
Muonekano wa sehemu ya The Robi’ s Bar & Grill
Muonekano wa sehemu ya The Robi’ s Bar & Grill
Muonekano wa sehemu ya The Robi’ s Bar & Grill
Muonekano wa sehemu ya The Robi’ s Bar & Grill
Muonekano wa sehemu ya The Robi’ s Bar & Grill
Wadau wakifuatilia Mpira wa miguu  kupitia Screen The Robi’ s Bar & Grill
Karena  conference center
Karena Hotel
Karena Hotel
Hennessy
 
 

About the author

mzalendoeditor