Mhe. Jaji (Mst) Sivangilwa Mwangesi Kamishna wa Maadili (wa kwanza kushoto) na Bw. John Kaole Katibu Usimamizi wa Maadili (kushoto kwa Jaji Mwangesi) wakiweka shada la maua katika kaburi la Benny Kabungo eneo la Nonde jijini Mbeya tarehe 30 Machi, 2023. Benny alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu katika Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Mhe. Jaji (Mst) Sivangilwa Mwangesi Kamishna wa Maadili tarehe 30 Machi, 2023 akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Benny Kabungo aliye kuwa Mkurugenzi wa Utawla na Rasilimaliwatu mtaa wa Jakalanda jijini Mbeya. Kabungo alifariki dunia tarehe 27 Machi, 2023.