Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI SAGINI ASHIRIKI KATIKA ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI, GEITA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Sagini akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Maambukizi ya VVU na UKIMWI Gereza la Wilaya Geita kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI, leo katika ukumbi wa Maonesho ya Dhahabu EPZ, Mkoani Geita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Dawa za Kulevya, KIfua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza Mhe. Fatma Taufiq (Mb.) akiongoza kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI yanayoendelea leo katika ukumbi wa Maonesho ya Dhahabu epz, Mkoani Geita. Pembeni kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini.

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Mhe. Constatine Kanyasu,akichangia jambo kuhusu Taarifa ya Hali ya Maambukizi ya VVU na UKIMWI Gereza la Wilaya Geita leo, iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo, kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI katika ukumbi wa Maonesho ya Dhahabu epz, Mkoani Geita.

Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Christina Mnzava akiwasilisha hoja juu ya Taarifa ya Hali ya Maambukizi ya VVU na UKIMWI Gereza la Wilaya Geita leo, iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo, kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI katika ukumbi wa Maonesho ya Dhahabu EPZ, Mkoani Geita.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI ambao pia ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizowasilishwa nao leo,katika ukumbi wa Maonesho ya Dhahabu, EPZ , Mkoani Geita.

Naibu Waziri,Jumanne Sagini akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI, Mhe. Fatma Taufiq (Mb.) (katikati) na baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wakijitayarisha kuelekea Gereza la Wilaya Geita,leo kufahamu changamoto za wafungwa na mahabusu wa gereza hili ili kuyapatia suluhisho.

About the author

mzalendoeditor