MABINGWA Watetezi Timu ya Yanga imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kuchukua taji la 29 baada ya kuwachapa wenyeji KMC bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu NBC ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam
Katika mchezo huo Yanga Sc iliwapumzisha nyota wao waliocheza kwenye mechi ya Kimataifa akiwemo Mayele, Bangala, Moloko, Job, Lomalisa, Mudathir, Pamoja na Aucho.
Yanga sc ilianza kupata bao dakika ya 38 ya mchezo kupitia kwa nyota wao kinda Clement Mzize ambaye alianza na baadae kumpisha Fiston Mayele kipindi cha pili kwenye mchezo huo.
Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 62 na kuiacha Simba SC kwa tofauti ya pointi 8 timu zote zikiwa zimecheza mechi 23.