Featured Kitaifa

DK.MOLLEL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA HALMASHAURI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

NAIBU  Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel ,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya Prof Abel Makubi,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

NAIBU  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) anayeshughukia afya Dkt. Grace Magembe ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

 

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Waganga Wakuu wa Mikoa Tanzania Dkt. Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema  kuna haja ya  kuandaa na kutengeneza mfumo mmoja wa kidigitali utakaounganisha huduma za afya zote nchini ili kuwezesha ufanisi wa kiutendaji katika sekta ya afya.

Hayo ameyasema  wakati  akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.

 Dk. Mollel amesema  kuwa  kuna haja ya kutengeneza mfumo mmoja wa kidigitali utakaounganisha huduma za afya nchini.

“Tuna mifumo mingi ambayo wakati mwingine inachanganya na inatushinda kutumia, niwaombe maafisa TEHAMA wa Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI watutengenezee mfumo mmoja ili tupunguze mikanganyiko ya mifumo hii mingi” amesema Dk.Mollel

“Tunatakiwa kuwa na mfumo mmoja ambao kipimo cha CT-Scan kikifanyika Mtwara mtu wa makao makuu ataona, dawa zikitolewa Kigoma zitaonekana kwenye mfumo, hii itatusaidia kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia itatuondolea mkanganyiko na kuzuia upotevu wa dawa na vifaa tiba” ameongeza

Aidha Dk. Mollel amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) kuhakikisha kuwa anapeleka vifaa tiba na dawa mahospitalini ndani ya saa 24 baada ya kupokea fedha kutoka serikali kuu ili kuboresha hali ya utoaji na upatikanaji huduma za afya.

Dk. Mollel amesema kuwa ili kuboresha huduma za afya ni lazima kuwepo kwa dawa na vifaa tiba vya kutosha katika maeneo ya kutolea huduma.

“Mkurugenzi uko hapa na umesikia, kuna wakati hospitali zina fedha zao mkononi lakni MSD hana dawa ila kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi dawa zipo, Serikali imefanya kazi kubwa sana ya ujenzi wa miundombinu lakini vituo vingi havifanyi kazi kwa sababu ya ukosefu wa vifaa tiba na dawa, tukitoka hapa MSD mliangalie hili vizuri na kuhakikisha baada ya malipo dawa zinatolewa ndani ya saa 24” amesema Dk. Mollel.

Akijibu pia hoja ya kuwepo kwa changamoto ya gharama kubwa za matibabu zinazowashinda wagonjwa kumudu Naibu Waziri Dk. Mollel alisema kuwa dawa pekee ya kukabiliana na changamoto ya gharama za matibabu kwa wananchi ni kupitishwa kwa sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

Akijibu risala hiyo, Dkt. Mollel amesema ni kweli kumekua na malalamiko makubwa ya wananchi kutokupata huduma zinazokidhi viwango kupitia kadi za CHF.
“Kila ninapofanya ziara kwenye  Mikoa na Wilaya napokea malalamiko  juu ya madhaifu mkubwa wa CHF na wananchi wanadhani ndio kadi za Bima ya Afya ya Taifa ya (NHIF)” amesema, Dkt. Mollel.
“Nakiri kuwa CHF ni tatizo kila mahali hata huko nilikifanya ziara wananchi wanalalamikia CHF na wengi wanasema BIMA YA AFYA ukiwambia leteni kadi zenu wanaleta za CHF ambazo siyo NHF” amesisitiza
Dkt. Mollel
Dkt. Mollel amesema njia muafaka ya kuondokana na kero na malalamiko ya wananchi kwenye upatikanaji wa huduma ni kupitia muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote utaotoa nafasi kwa wananchi kupata huduma bora katika hospitali zote nchini kuanzia zahanati mpaka hospitali ya taifa.

Kwa upande wake  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kuwa ni vyema mifumo ya kimtandao ikapunguzwa kupitia eGa ikabaki mifumo michache itakayoweza kuwasiliana ili kurahisisha utendaji kazi na uboreshwaji wa huduma za afya nchini.

 Awali akisoma hotuba ya Waganga Wakuu, Mwenyekiti wa Waganga wakuu wa Mikoa (RMO’s) Dk. Best Magoma amesema kuwa mpaka kufikia mwezi Januari mwaka huu tayari serikali imeipelekea MSD Bilioni 129 tsh/- sawa na asilimia 68 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2013 ambayo ni Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa Dawa na vifaa tiba.

 

 

About the author

mzalendoeditor