Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt.Silas Wambura akizungumza katika kuhitimisha Mafunzo ya Siku tano ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID UZAZI STAHA Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Afisa Program huduma za afya ngazi ya jamii ,Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya Orsolina Tolage akizungumza katika kuhitimisha Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID UZAZI STAHA Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [OR-TAMISEMI]Martha Mariki akizungumza katika kuhitimisha Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID UZAZI STAHA.
Dkt.Rebecca Mdee Mwezeshaji Kiongozi Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID UZAZI STAHA akitoa Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 5 katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi[FDC]kwa kushirikisha Asasi za Kiraia kutoka baadhi ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza na Shinyanga ambazo ni Magu,Sengerema,Ukerewe ,Misungwi,Msalala,Kishapu na Manispa ya Shinyanga.
Baadhi ya wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia wakiwa katika Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID UZAZI STAHA siku ya tano Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema Mkoani Mwanza.
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza,Dkt.Silas Wambura akiwa picha ya pamoja na Afisa Program huduma za afya ngazi ya jamii ,Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya Orsolina Tolage ,upande wa kushoto ,Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [OR-TAMISEMI]Martha Mariki upande wa kulia akifuatiwa wakifuatiwa na wawakilishi wa Americares mwishoni upande wa kulia na kushoto pamoja na wawakilishi wengine wa Asasi za Kiraia kutoka mikoa ya Mwanza kwa halmashauri ya Magu,Sengerema,Ukerewe na Misungwi na Mkoa wa Shinyanga kwa Halmashauri ya Msalala,Kishapu na Manispaa ya Shinyanga katika hitimisho kwa mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa USAID UZAZI STAHA.
Na.Faustine Gimu,Elimu ya Afya kwa Umma
Imeelezwa kuwa Tathmini shirikishi ya Kijamii[Community Score Card] imekuwa mwarobaini katika kupunguza changamoto za Huduma ya Afya katika jamii na kuweza kuleta mabadiliko chanya katika ubora wa huduma .
Hayo yamebainishwa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza na Afisa Program Huduma za Afya ngazi ya Jamii,Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma ,Idara ya Kinga ,Wizara ya Afya Orsolina Tolage katika ufungaji wa Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) kwa Asasi za Kiraia katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa Usaid Uzazi Staha.
Tolage amesema kupitia Mafunzo hayo ,Timu za Uendeshaji na Usimamizi Huduma za Afya za Halmashauri(CHMTs )pamoja na Asasi za Kiraia ni muhimu kushirikisha jamii ni namna gani huduma za afya inapokea .
“Mojawapo ya kushirikisha jamii ni pamoja na kutumia Community Score Card na kubaini viashiria vipi vinaonesha changamoto za Afya na wananchi kuweza kupima ni kiashiria kipi hakijafanya vizuri na kuweza kuboresha”amesema.
Aidha,Tolage amesema kupitia Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii wamejiwekea Mpango Kazi utakaokuwa unapimwa hatua za utekelezaji baada ya miezi mitatu na kuona mabadiliko yapi yametokea.
“Tumeweka Mpango Kazi baada ya miezi mitatu ufuatiliaji unafanyika ndani ya kituo ni mabadiliko yapi yametokea katika uboreshaji wa huduma na tutaendelea ufuatiliaji na baadhi ya vitu vinakuwa ndani ya uwezo wa wananchi wenyewe pamoja na maeneo husika ya utoaji wa huduma pia serikali imeandaa Mwongozo na itaendelea kuuboresha kufikia mwaka wa fedha 2023/2024 mwongozo huu utakuwa umekamilika”amesema.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Silas Wambura ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Ufungaji wa Mafunzo hayo amesema Tathmini Shirikishi ya Kijamii ni muhimu kwani jamii ndio kioo kinachopima hali halisi ya upatikanaji wa huduma ngazi ya jamii husika.
“Ukitaka kujipima kama unatoa huduma Bora ni Tathmini kwa wanannchi ,ni kioo chetu hivyo wananchi kujitathmini wao wenyewe na huduma zinazotolewa katika maeneo yao ni kitu cha muhimu sana ili kuweza kubaini changamoto zilizopo na serikali iweze kuzifanyia kazi”amesema.
Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [OR-TAMISEMI]Martha Mariki amesema Tathmini Shirikishi ina umuhimu mkubwa hivyo kuna haja ya kufika katika maeneo mengine na kubainisha kuwa dawa na majengo peke yake haitoshi kujipima kuwa huduma bora inatolewa kwa mwananchi .
“Tuna kazi kubwa kuhakikisha afua hii tunapeleka katika maeneo mengine ambapo itawezesha kuwapa mafunzo wataalam ,kwa hiyo kuwa na majengo na dawa hakutoshi kupima kuwa unatoa huduma bora hivyo hatua hii ya tathmini shirikishi ya Jamii ndio inayotupa mwanya wapi panahitaji marekebisho katika uboreshaji wa huduma”amesema.
Mratibu wa Uhusiano Jamii na Mabadiliko ya Tabia kutoka Americares Mussa Lunyonga amesema Mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Jamii (Community Score Card) yametolewa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wakufunzi wabobezi wa Tathmini Shirikishi.
Ikumbukwe kuwa Mafunzo hayo ya tathmini shirikishi ya jamii sekta ya afya yametolewa kwa Asasi za Kiraia kutoka mikoa ya Mwanza kwa halmashauri ya Magu,Sengerema,Ukerewe na Misungwi na Mkoa wa Shinyanga kwa Halmashauri ya Msalala,Kishapu na Manispaa ya Shinyanga.