Featured Michezo

SIMBA YAICHAPA SINGIDA BIG STAR

Written by mzalendoeditor

NA EMMANUEL  MBATILO,  DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeendelea kuuwasha moto  kwenye ligi ya NBC hasa kwa kutoa dozi za uhakika kwa timu za ligi hiyo ambapo leo imefanikiwa kuichapa timu ya Singida Big Star kwa mabao 3-1.

Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, tumeshuhudia mshambuliaji raia wa Congo Jean Baleke akiweka kambani tena kwa mara nyingine tokea alivyojiunga na miamba hiyoya msimbazi.

Haikuishia hapo tu,  nyota wa timu hiyo  Saidi Nitbazonkiza nae alifanikiwa kuingia kambani tena kwa kufunga bao la pili kwenye mchezo  huo  ambalo liliwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1 huku bao pekee la Singida Big Star likifungwa na Bruno Gomez

Bao la tatu la Simba Sc lilifungwa na Osman Sakho akipokea krosi kutoka kwa Shomari Kapombe, bao  ambalo   liliwashua mashabiki wengi kwani  linataka kufanana na lile ambalo alifunga kwenye michuano ya CAF mwaka jana.

About the author

mzalendoeditor