Featured Michezo

YANGA YA MOTO,MAYELE HASHIKIKI LIGI KUU YA NBC

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo-Mzalendo blog

MABINGWA Watetezi Yanga wameichapa mabao 2-0 Mbeya City na kufikisha Mechi 49 bila kupoteza mchezo wowote kwenye Ligi Kuu na kuendelea kuongoza Msimamo wa Ligi mchezo uliiopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilipata mabao yote mawili kupitia kwa mshambuliaji hatari kunako Ligi Kuu Fiston Mayele mnamo dakika ya 24 na 79.

Mayele amefunga mabao saba katika mechi tatu za Ligi na kuongoza msimamo wa wafungaji kwa kufikisha jumla ya mabao 10 huku akiwa na mechi moja mkononi.Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha pointi 32 wakiwa wamecheza mechi 12,Azam FC wakishika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 29 wakicheza mechi 13 huku Simba ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 28 wakiwa wameshuka dimbani mara 13.

Ligi hiyo itaendelea kesho vigogo wa Soka wekundu wa Msimbazi Simba watashuka katika uwanja wa Ushirika Moshi kucheza na wenyeji Polisi Tanzania majira ya saa kumi jioni na Azam FC watacheza na Coastal Union uwanja wa Chamzi majira ya saa moja usiku.

About the author

mzalendoeditor