Washiriki wa kikao kazi cha mafunzo ya uwezeshaji kitaifa juu ya namna kujenga uwezo wa kuibua hadithi za mafanikio miongoni mwa walimu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni wakisikiliza nasaha za Katibu mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael.
……………………………
Na Farida Mangube.Morogoro.
Watumishi wa kada ya elimu wapatao 6986 kutoka katika halmashauri 29 za mikoa ya Katavi, Kigoma, Singida na Pwani, wanatarajiwa kupatiwa mafunzo ya walimu kazini yatakayo husisha maafisa elimu wa mikoa na wilaya, wadhibiti ubora wa shule kanda na halmashauri, maafisa elimu kata, walimu wakuu, walimu wa taaluma pamoja na walimu wa ashule za msingi.
Hayo yameelezwa na Katibu mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael kwenye kikao kazi cha mafunzo ya uwezeshaji kitaifa juu ya namna kujenga uwezo wa kuibua hadithi za mafanikio miongoni mwa walimu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni.
Dkt.Michael alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuboresha ujifunzaji na ufundishaji kwa wanafunzi katika shule zoti nchini ikiwa ni poamoja na wanafinzi wenye mahiaji maalumu.
Aidha alisema kuwa kupitia programu ya shule bora mafunzo yamekwishafanyika katika Halmashau 29 za mikoa ya Mara, Kigoma, Singida, Simiyu, Dodoma, Tanga pamoja na Rukwa kwa maafisa taaluma wa Wilaya, wadhibiti ubora wa shule, Waratibu wasaidizi wa Tume ya utumishi wa walimu, walimu wakuu, walimu wa taaluma pamoja na wawezeshaji rika.
“Mafunzo yalilenga kujenga uwezo wa kusimamia na kuendesha mafunzo endelevu kwa walimu kazini lakini pia kufuatilia utekelezaji wa mtaala wa elimu ya msingi kwa kutumia hadithi za mafunzo za kujifunza zitakazokuwa kichocheo kwa walimu wengi kujifunza hadithi hizo” alisema Dkt.Michael
Hata hivyo amewaagiza watumishi hao kutekeleza kikamilifu jukumu la kutoa mafunzo hayo kwa umakini mkuwa na kwa kuhakikisha kuwa lengo kuu la mafunzo hayo linafikiwa ipasavyo.
“Uwekezaji katika mafunzo haya ya walimu kazini ni mkuwa sanahi vyo nawaagiza viongozi katika nazi zote kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mafunzo pamoja na kuweka mikakati na mipango endelevu katika mamlaka zao na kuhakikisha kuwa mafunzo yanakuwa na tija na uendelevu kwa awalimu” alisema Dkt.Michael
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dk.Aneth Komba. aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia nafasi na muda wanaotumia katika mafunzo kupata ujuzi utakao wasaidia kwenda kuleta mabadiliko chanya katika elimu ya Tanzania.
Pamoja na mambo mengine Dk.Aneth Komba. alisema kuwa ili kuweza kuandaa moduli zinazokidhi mahitaji kazi mojawapo ni kukusanya na kufanya tathmini ya mahitaji halisi ya walimu ambayo hata hivyo yanatofautiana kutoka shule moja kwenda nyingine.