Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUZINDUA MRADI WA VIHENGE VYA KUHIFADHIA MAZAO BABATI.

Written by mzalendoeditor

Na John Walter-Manyara

Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mradi wa Vihenge nane mjini Babati wenye uwezo wa kuhifadhi tani 25,000 za mazao.

Akitoa taarifa hiyo afisa mtendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa  amesema mradi huo uliojengwa kisasa umekamilika kwa asilimia 100 na vina uwezo wa kutunza chakula kwa muda wa zaidi ya miaka mitano bila kuharibika.

Amesema Rais Samia akiwa katika ziara mkoani Manyara Jumanne  Novemba 22,2022 atazindua rasmi mradi huo uliogharimu Bilioni 19 na milioni 359
Kukamilika kwa mradi huo ni fursa kwa ukanda wa Arusha,Kilimanjaro na Manyara kuhifadhi tani 70,000 za mazao ikiwa ni kiwango kikubwa kilichoongezeka ikilinganishwa na tani 39,ooo za uhifadhi wa hapo awali.

Aidha lupa ameongeza kuwa licha ya vihenge nane kujengwa lakini pia mradi umehusisha ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 15 ikifanya idadi ya jumla ya uhifadhi wa vihenge na maghala kuwa tani 40,000.

Lupa ameeleza changamoto mbalimbali walizokutana nazo hadi kukamilika kwa mradi ikiwemo ugonjwa wa UVIKO 19 baada ya mkandarasi kushindwa kuendelea na mradi kutokana na hofu ya mkandarasi huyo kutoka nje ya nchi kuchangamana.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Babati na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi hapo katika uzinduzi huo.

About the author

mzalendoeditor