SIMBA SC imerejea Kileleni Kibabe baada ya Kuizamisha mabao 4-0 Timu ya Ruvu Shooting Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukaa mechi nyingi bila kufunga bao Mshambuliaji John Bocco amefufuka dhidi ya Ruvu Shooting kwa kufunga Hat-Trick yake ya kwanza ikiwa ya Pili Msimu wa Ligi mara baada ya Mayele kupiga hat-Trick dhidi ya Singida Big Star.
Bao lingine limefungwa na beki Shomary Kapombe na kwa ushindi huo Simba wamerejea kileleni kwa kufikisha Pointi 27 na kuishusha Yanga hadi nafasi ya pili wakiwa na Pointi 26 nafasi ya tatu wakishika nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 26,Simba na Azam FC wakiwa wamecheza mechi 12 kila moja na Yanga wakiwa wamecheza mechi 10.
Ligi hiyo itaendelea kesho Matajiri wa jiji la Dar es Salaam kutoka Chamazi Timu ya Azam FC itashuka ugenini kucheza na Wauaji wa Kusini Namungo FC katika uwanja wa Majaliwa Mkoani Lindi majira ya saa moja usiku.