Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Leo tarehe 12 Novemba 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. (Picha na CCM Makao Makuu)
..……………………………..
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, leo tarehe 12 Novemba, 2022 Dodoma. Kikao hiki ni maandalizi ya kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) kitakacho fanyika siku ya kesho tarehe 13 Novemba, 2022.
Pamoja na mambo mengine vikao hivi vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama walioomba uongozi katika ngazi ya mikoa na taifa kwa upande wa jumuiya pamoja na chama.