Featured Michezo

YANGA YAENDELEZA UNBEATEN,YAICHAPA GEITA GOLD CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Written by mzalendoeditor

Na Odilo Bolgas,MZALENDO BLOGS

MABINGWA  wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara timu ya  Yanga  imeendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika mechi 45 za ligi baada ya  kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Shujaa wa Yanga ni Winga mtukutu Bernard Morrison aliipatia bao timu yake mnamo dakika ya 45  kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira ndani ya 18.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 20 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.

Mchezo mwingine umepigiwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Tanzania Prisons imenusurika kufungwa na Namungo FC baada kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1

About the author

mzalendoeditor