Featured Kimataifa

RAIS WA UKRAINE AGOMEA MAZUNGUMZO NA URUSI KUFANYIKA BELARUS

Written by mzalendoeditor

Wakati wajumbe wa Urusi wakidaiwa kuwasili nchini Belarus tayari kwa mazungumzo na Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekataa ombi hilo, akisema mazungumzo ya Minsk yangewezekana ikiwa Urusi isingeishambulia Ukraine kutokea eneo hilo la Belarus.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza BBC, hata hivyo Rais huyo wa Ukraine ameacha mlango wazi wa mazungumzo katika maeneo mengine aliyosema hayatumiki kurushiwa makombora dhidi yao na anaamini hiyo eneo hilo linaweza kuwa na mazungumzo ya kweli ya kumaliza vita hivyo vinavyozidi kushika kasi.

“Bila shaka tunataka amani, tunataka kukutana, tunataka vita viishe. Warsaw, Bratislava, Budapest, Istanbul, Baku – tumewapa Warusiā€¯ amenukuliwa akisema hayo rais wa Ukraine.

Rais huyo ameongeza kuwa, “Kama hakungekuwa na hatua kali kutoka kwa eneo lenu, tungeweza kuzungumza Minsk… miji mingine inaweza kutumika kama mahali pa mazungumzo.

Katika hatua nyingine Rais huyo wa Ukraine amewaalika wageni kupigana na ‘wahalifu wa kivita wa Urusi.’

Rais Zelensky alitoa wito huo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimkaribisha mtu yeyote kuja kupigana “bega kwa bega” na Waukreni.

“Yeyote anayetaka kujiunga na ulinzi wa Ukraine, Ulaya na dunia anaweza kuja na kupigana bega kwa bega na Waukraine dhidi ya wahalifu wa vita wa Urusi.”

About the author

mzalendoeditor