AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) CPA.Milton Lupa,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 22,2022 jijini Dodoma.
…………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) imeanza kupeleka chakula cha bei rahisi katika halmashauri tisa nchini zenye mfumuko mkubwa wa bei za vyakula.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 2,2022 jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) CPA.Milton Lupa, wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
CPA. Lupa amesema ili kukabiliana na makali ya mfumuko wa bei za nafaka Wakala kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo imeongeza upatikanaji wa nafaka katika masoko ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi.
”Wakala unahudumia Halmashauri za Bunda, Sengerema, Geita, Nzega, Liwale, Nachingwea, Longido, Loliondo na Monduli ambapo takriban tani 3,000 zimepelekwa katika maeneo hayo.”amesema CPA.Lupa
Aidha amesema kuwa Wakala imejipanga kuhudumia maeneo mengine yatakayothibitika kuwa na mahitaji ya dharura au upungufu wa Chakula.
Ameeleza kuwa wakala unatekeleza Mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka ambapo mradi huo ukikamilika utaongeza uwezo wa kuhifadhi kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000.
AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) CPA.Milton Lupa,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 22,2022 jijini Dodoma.
AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) CPA.Milton Lupa,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasilisha taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 22,2022 jijini Dodoma.