Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU:’TUTAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATOTO WA KIKE’

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kuwezesha Vipaumbele vya Wanawake na Wasichana katika Mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam.

………………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele katika kuhakikisha wanawake na watoto wa kike wanapata huduma wezeshi zikiwemo za afya na elimu ili kuwezesha kujenga jamii yenye usawa.

Amesema Serikali inatambua na itaendelea kuunga mkono jitihada za Mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Umoja wa Kimataifa la Wanawake kwa kuendelea kutunga kuboresha Sera za usimamizi wa usawa wa kijinsia ili kumuwezesha mtoto wa kikekufikia malengo yake.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 10, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Viongozi wa Ngazi za Juu ya Kuwezesha Viongozi Wakuu juu ya Kuwezesha Vipaumbele vya Wanawake na Wasichana katika Mapambano Dhidi ya Virusi Vya Ukimwi uliofanyika Serena Hoteli jijini Dar Es Salaam.

Amesema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wanaweka kipaumbele katika kuwahudumia wanawake wanaoishi na VVU ikiwemo kuviwezesha vikundi vyao, kutoa elimu pamoja na kuwajumuisha katika ngazi za maamuzi kwenye sehemu za kutolea huduma za afya

“Wasichana wakipata elimu bora wataweza kuepukana na maambukizi ya virsri vya ukimwi, kuanzia katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo ni wajibu wetu kuwekeza kwa watoto wa kike ili kuwa na jamii yenye mafanikio na usawa katika maendeleo.”

“Tunapaswa kuwaweka wanawake na watoto wa kike kwenye vipaumbele vyetu ili kueleta mabadiliko kwa jamii, lazima tusikilize sauti zao, na kuwapa nafasi katika ngazi za maamuzi na uongozi, kwa pamoja tunapaswa kuwawezesha mabinti wa kiafrika kufikia nafasi za uongozi.”

Waziri Mkuu amesema katika kufanikisha mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi ni vyema watoto wa kike wakapewa nafasi katika utungaji wa Sera na miongozo ya kupambana na ugonjwa huo itaongeza ufanisi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwani kundi hilo limekuwa sehemu ya waathirika wakubwa.

Mkutano huo umehudhuria na viongozi wanaohusika na masuala ya afya kutoka Tanzania, Botswana, Cameroon, Cote de Voir, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Africa Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe, ambao wamejadili  mbinu mbalimbali za kutatua changamoto za VVU ambazo zinaleta athari miongoni mwa watoto wa kike na wanawake vijana.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kuwezesha Vipaumbele vya Wanawake na Wasichana katika Mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, Oktoba 11, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)   

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa na UKIMWI Duniani, Winnie Byanyima baada ya kufungua mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kuwezesha Vipaumbele vya Wanawake na Wasichana katika Mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, Oktoba 11, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor