Na Eva Godwin,MZALENDO BLOG
MABINGWA Watetezi Yanga wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa mabao 2-1 Ruvu Shooting Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana kutokana na Ruvu Shooting kucheza kwa kujilinda zaidi.
Kipindi cha Pili timu zote zilifanya mabadiliko na Yanga wakiendelea kuutawala mchezo huo mnamo dakika ya 52 Fiesal Salum ”Fei Toto”aliwanyanyua mashabiki wake.
Kapteni wa Yanga Bakari Mwamnyeto alifunga bao la pili akifunga kwa kichwa na Ruvu Shooting walipata bao la kufutia machozi likifungwa na Roland Msonjo dakika ya 85.
Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 13 wakiwa nafasi ya pili huku Simba wakiongoza Ligi wakiwa na Pointi 13 sawa na Yanga huku Simba akiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Mchezo mwingine umechezwa Mkwakwani Tanga wenyeji Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.