Featured Kitaifa

UVCCM YATOA ONYO KWA WAGOMBEA

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa Khenan Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 3,2022 jijini Dodoma kuhusu mwenendo wa changuzi mbalimbali ndani ya jumuiya.

…………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),kimewataka watia nia kutambua hakuna mwenye mamlaka ya kuteua wagombea isipokuwa vikao vya chama na jumuiya zake.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 3,2022 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa Khenan Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa changuzi mbalimbali ndani ya jumuiya.

Amesema kuwa mgombea atakayekwenda kinyume na utaratibu, tamaduni na kanuni zinazoongoza chama kwani atakosa sifa ya kuteuliwa akibainika na vitendo hivyo.

”Hivyo asitokee mtu au kikundi cha watu kikajipa mamlaka ya kufanya kazi ya vikao nje ya utaratibu watakuwa wamepoteza sifa ya kuteuliwa. ”amesema  Kihongosi 

Ameeleza kuwa kuanzia Oktoba 8 mwaka huu, kutakuwa na usahili kwa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na na waliogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ndani ya chama kitaifa.

“Hivyo wagombea wanatakiwa kuja na viambatanisho kama cheti cha kuzaliwa, kadi ya uanachama wa CCM na UVCCM, vyeti vya masomo na mafunzo mbalimbali, kadi ya Nida au namba maana lazima tuhakiki umri wa mgombea.”amesema

About the author

mzalendoeditor