Waziri wa Nchi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene,akizungumza na wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wazee yaliyofanyika leo Oktoba 03, 2022 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imeziagiza mamlaka za Serikali za Mitaa kuwashirikisha Wazee kupitia mabaraza yao kushiriki kwenye vikao vya maamuzi kuanzia ngazi za vijiji na mitaa hadi Mabaraza ya Madiwani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene,wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wazee yaliyofanyika leo Oktoba 03, 2022 kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mhe. Majaliwa amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Jamii inawatambua na kuwathamini wazee ikiwemo kuanzisha Kampeni ya mpishe Mzee kwenye maeneo mbalimbali ya kutolea Huduma.
“Kila Halmashauri iweke maeneo mazuri ya kukaa wakati wa mikutano ya mabaraza ya Madiwani na Wazee wanapo jadili mambo yao mzingatie Uzalendo na ujenzi wa maadili mema kwa watoto wetu” amesema Simbachawene
Simbachawene amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua Makundi muhimu hususani Wazee kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya kushughulikia Makundi hayo kwani kabla
Makundi hayo yalikuwa ,yanakosa mahali maalum pa kupeleka Masuala yao .
Ameongeza kwamba, Serikali inaendelea kuelimisha jamii kuzingatia ulinzi na usalama kwa Wazee Kwa kuanzisha mabaraza ya wazee 20749 Kwa lengo la kuwapa fursa ya kujadili mambo yao na kuwa chombo cha kushauri Jamii.
Waziri Simbachawene ametumia nafasi hiyo kutoa Rai kwa viongozi na Wazee kuwa pamoja na kutumia mabaraza hayo kujadili Ustawi wao wahakikisha umoja na Jumuiya nyingine za Wazee zinatambuliwa na kusajiliwa katika maeneo yao na taarifa za utekelezaji wa mabaraza ya Wazee zijumuishwe kwenye kamati za Maendeleo ili mawazo yao yaweze kuzingatiwa na kufanyiwa kazi.
Ametoa wito kwa Jamii kushirikiana kuzuia ukatili kuliko kunyamaza na hatimaye kunung’unuka na kuombolea matukio yanapotokea.
Awali Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema maadhimisho hayo ni matokeo ya maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzisha Wizara hii.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amesema kuwa, TAMISEMI imeendelea na zoezi la kuwatambua wazee na hadi sasa imetambua 2117637 kutoka Mikoa yote 26 bapo wanaume ni 1382468 na wanawake 735169.
“Tumetoa Bima ya Afya ya Jamii kwa Wazee ili wapate huduma kwenye vituo vya Afya ngazi ya msingi kuanzia zahanati Hadi hospitali za Wilaya” amesema Dkt. Grace.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe Stanslaus Nyongo amesema wabunge wapo tayari kuhakikisha mchakato wa kupitia sera ya Wazee na kutungiwa sheria ya Wazee unakamilika.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Mzee Lameck Sendo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi kubwa anayoifanya ikiwemo miradi mikubwa, kuhamasisha Utalii ambapo mingi imeongeza ajira kwa vijana.
“Jumla ya mabaraza 20749 yameundwa tunaendelea kuimarisha Mawasiliano Kwa mabaraza yote na kupata taarifa kwa muda mfupi” amesema Mzee Sendo.
Wazee wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene,akizungumza na wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wazee yaliyofanyika leo Oktoba 03, 2022 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akitoa salaam za Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akieleza mikakati ya Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe,akizungumzia mikakati ya Wizara ya TAMISEMI jinsi inavyozidi kuboresha mazingira ya wazee nchini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe Stanslaus Nyongo,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa taarifa za Mkoa wa Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Mzee Lameck Sendo,akitoa taarifa ya wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee iliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
Wazee walioshiriki maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wazee wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika Maadhimisho yaliyofanyika Kitaifa leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu Mhe. George Simbachawene akitoa msaada wa vifaa kwa baadhi ya Wazee kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee yaliyofanyika leo Oktoba 03, 2022 Jijini Dodoma.