Featured Kitaifa

BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA KWA AJILI YA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MAMA SAMIA KAHAMA

Written by mzalendoeditor
 
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi meza Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Meza hiyo ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021. 
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Benki ya CRDB imekabidhi viti 62 na meza 62 kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika mtaa wa Sokola kata ya Majengo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
 
 
Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo Jumanne Septemba 27,2022 katika shule hiyo ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi viti na meza hizo, Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema benki hiyo ni mdau mkubwa wa elimu na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika shule ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
“Leo tunakabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Samia ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa benki ya CRDB kushirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu. Tutaendelea kushirikiana na serikali kutatua changamoto zilizopo”, amesema Wagana.
“Sisi Benki ya CRDB kama Benki inayoongoza nchini Tanzania tunaamini suala la elimu ni la kila mtu, tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia mahitaji yaliyopo katika shule zetu kwani serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zote”, ameongeza.
Katika hatua nyingine Wagana ametumia futsa hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB ikiwemo mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima na watumishi pamoja na kufungua akaunti zikiwemo akaunti kwa ajili ya watoto ‘Junior Jumbo Account’ na Malkia Account kwa ajili ya wanawake.
 
 
“Sisi CRDB tunajitahidi kuwezesha watoto wasome katika mazingira bora na tutaendelea kuboresha sera zetu. Benki ya CRDB ni mahali salama, tuna akaunti za kila aina, karibuni mtuunge mkono kwenye benki hii ya Watanzania”, ameeleza Wagana.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kahama, Evodi Kareti na Meneja Rasilimaliwatu Benki ya CRDB, Benjamini Ngaiwa wamewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha washindwe kumaliza masomo hivyo kutotimiza ndoto zao na kwamba Benki ya CRDB itaendelea kutoa michango mbalimbali katika sekta ya elimu.
Akizungumza wakati wa kupokea viti na meza hizo, Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya ameishukuru Benki ya CRDB kwa namna inavyoendelea kushirikiana na serikali kutatua changamoto katika sekta ya elimu huku akibainisha kuwa viti na meza hizo zitasaidia wanafunzi hao kusoma katika mazingira bora.
 
“Tunawashukuru benki ya CRDB kwa kuendelea kutushika mkono, naomba mtunze viti na meza hizi pamoja na miundombinu mingine ya shule”, amesema Ndanya.
Aidha amewashukuru wananchi wakiwemo wafanyabiashara kufungua akaunti katika benki ya CRDB kwani benki ikipata wateja wengi itapata faida na kurudisha faida hiyo kwa wananchi.
Ndanya ameipongeza shule ya sekondari Mama Samia kwa kutokuwa na rekodi ya mimba kwa wanafunzi hivyo kuwataka wanafunzi hao kujitunza na kujiheshimu na kuachana na vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao.
Awali akizungumza, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mama Samia, Joyce Thomas Jewe ameishukuru Benki ya CRDB kutatua changamoto ya uhitaji wa viti na meza katika shule hiyo changa iliyoanzishwa Tarehe 05.05.2021 ambayo sasa ina jumla ya wanafunzi 547 kati yao wasichana ni 267 na wavulana ni 284 ikiwa na walimu 15 kati yao wa kiume ni wawili na wa kike 13.
 
“Kutokana na uchanga wa shule hii tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mashine ya kuzalishia mitihani ya majaribio (Photocopy Mashine) na wamekwama kumalizia boma la jengo la utawala kwa kukosa nondo,kokoto na mifuko ya saruji ili pindi ujenzi utakapokamilika shule ipate mahali salama pa kutunzia nyaraka muhimu”,amesema.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi meza Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Meza hiyo ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021.  Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi  kiti Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Kiti hicho ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (kushoto) akimkabidhi kiti Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mama Samia iliyopo katika Manispaa ya Kahama. Kiti hicho ni sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana na Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya  na viongozi mbalimbali pamoja na wanafunzi wakipiga picha wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Muonekano wa sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Muonekano wa sehemu ya meza 62 na viti 62 vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja  Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja Rasilimaliwatu Benki ya CRDB, Benjamini Ngaiwa akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kahama, Evodi Kareti akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Diwani wa kata ya Majengo Manispaa ya Kahama, Benard Mahongo akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mama Samia , Joyce Thomas Jewe akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Afisa Elimu Manispaa ya Kahama, Anastazia Vicent akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia iliyoanzishwa mwaka 2021.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Samia wakifuatilia nasaha mbalimbali wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia 
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Samia wakifuatilia nasaha mbalimbali wakati Benki ya CRDB ikikabidhi meza 62 na viti 62 kwa ajili ya shule ya Sekondari Mama Samia 
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kahama, Evodi Kareti akizungumza na Wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Samia
Awali vijana wa Skauti wakimpokea mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akiwasili katika shule ya sekondari Mama Samia
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Samia.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
 

About the author

mzalendoeditor