Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wanachama wa CCM katika mkutano wa ndani akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
……………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Geita
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu amewashauri wabunge na madiwani wa Chama hicho kuwa wakali katika kuisimamia Serikali ili itekeleze ahadi za miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Kinana alitoa kauli hiyo jana mbele ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi aliokuwa anazungumza nao kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika Ofisi ya Chama hicho.
Alikuwa akielezea kwa kina namna ambavyo kuna baadhi ya miradi ikiwemo ya maendeleo ambayo inatengewa fedha lakini fedha hizo zinaelekezwa sehemu nyingine.
“Mimi ni mmoja wa watu ambaye ninapenda Wabunge wawe wakali kidogo kuhusu mambo ya Serikali, sio wakali kwa maana ya kuisakama Serikali lakini wawe wakali kwa kuiwajibisha serikali.
“Unajua hiki Chama ndicho kinachokwenda kwenye Uchaguzi , hiki Chama ndicho kinachoomba kura, hiki Chama ndicho kitakachopewa viongozi au kitakachonyimwa sio Serikali.Wale watendaji na watumishi wa Serikali wao wapo tu, wewe ukiwepo wao wapo, ukiondoka wao wapo,”alisema Kinana.
Aliongeza kuwa iwapo mambo hatakwenda watakaodhibiwa ni Chama Cha Mapinduzi , hivyo amewasihi lazima wana CCM wakiwemo madiwani na wabunge kuwa wakali.“Ndugu zangu nataka niwasihi sana lazima tuwe wakali na mambo ya wananchi, mambo yetu binafsi hatutakuwa wakali lakini mambo ya wananchi lazima tuwe wakali.”
Amefafanua hivyo katika kusimamia masuala yanayohusu maendeleo ya wananchi mbali ya kuwa wakali ni wajibu wa kila mmoja kwenye nafasi yake akatimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kumsaidia Rais katika kufanikisha malengo yake ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.
“Rais anajitahidi sana lakini Rais hayuko peke yake, Rais nchi hii si mali yake na katika uongozi lazima atumie taasisi, atumie taratibu, kanuni, sheria pamoja na sera na sisi wote tumsaidie Rais ili aweze kufanikiwa. Mmesema hapa(Geita)Rais ametoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo.
“Ametoa hiki, amesaidia kile lakini peke yake hawezi lazima Bunge, Kamati za Bunge, halmashauri, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri wasaidie na kila mmoja wetu asaidie upande wake.Hivyo tunaowajibu mkubwa sana,”alisisitiza Kinana.
Alifafanua kuwa CCM ndio inayopita na kuahidi wananchi kupitia Ilani kuhusu yatakayofanyika hivyo ahadi zinaposhindwa kutekelezwa wakati fedha zimetengwa wapinzani wanapita na kueleza CCM ahadi zao ni hewa.
“Kwa hiyo hapa Geita kwenye hili la ombi la kutengenezewa barabara nimejifunza na katika ziara zangu mikoa niliyokwenda nimekutana na hii la miradi kusua sua kwasababu ya fedha zinatengwa halafu hzipo,”aliongeza Kinana.
Akieleza zaidi kwenye hilo alisema atakwenda kukaa na Waziri wa Ujenzi ili amuulize swali kwamba ameona barabara fedha zinatolewa halafu baadae wanasema hazipo.
“Nilikuwa huko Rukqwa, Katavi na sasa hapa nyie (Geita) habari ndio hiyo hiyo, hata kama huna uwezo wa kutoa fedha zote basi toa kiasi fulani halafu tujue kwamba umeshindwa lakini uwaambie fedha hizi ilikuwa tutoe lakini zimekwenda mahala kwingine, hilo sio jambo jema sana.
“Na mengine ni kuzungumza na Mawaziri kama tunatoa fedha za barabara na tuangalie na mikoa ambayo haina barabara nyingi za lami, wale ambao barabara zao nyingi ni za lami basi kidogo wacheleweshwe na wale ambao hawana barabara za lami nyingi fedha ziende maeneo hayo.Sio maneno mazuri ya kusema lakini ni maneno ya ukweli,”alisema Kinana.
Alifafanua kuna mikoa ukienda barabara za lami ziko kila mahali lakini ukienda mikoa mingine unakuta hakuna barabara nyingi za lami lakini wakati wa kupanga bajeti za barabara za lami na kule kwenye barabara za lami.
KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI GEITA
Katika hatua nyingine Kinana alizungumzia migogoro ya ardhi mikoani Geita baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Mkoa ambayo imeteja eneo hilo kuwa na changamoto ya migogoro na kuomba Chama hicho kusaidia kumaliza migogoro hiyo.
“Mkuu wa Mkoa wa Geita jana na leo tumezungumza , nadhani hili jambo ni muhimu sana na lazima ifike mahali liishe, nchi hii ina migogoro mingi sana ya ardhi, kila mahali ardhi ardhi.Juzi nilikuwa Kigoma tulifanya mkutano kuanzia saa tisa mpaka saa 2:30 usiku na wana CCM.
“Nusu ya muda tumezungumzia ardhi na mgomvi mkubwa ni ardhi , ardhi, ardhi, sasa lazima tufike mahali tupate ufumbuzi, hapa kwenu(Geita) mna matatizo na misitu, mgororo kati ya wananchi na misitu , mgororo kati ya wananchi na hifadhi.Mgogoro huu sio wa leo.
“Mimi nikiwa Katibu Mkuu wa CCM na nilipita kote huko nimeiukuta .Rais amekua ameunda timu na imekuja hapa , mkuu wa Mkoa ameniambia imefanya kazi nzuri lakini kuna sehemu wameacha.Nitaandika kwenye taarifa zetu na kupeleka kwa Rais.
“Kuna wale watu uliowatuma kule hawajafika kila mahali halafu mtu anaulizwa mbona hamjafika kila mahali anajibu kumbe nimesahau.Sasa unasahau vipi wakati umetumwa na Mkuu wa nchi.Kwa hiyo lazima tutafute namna ya kupata ufumbuzi wa kutatua,”alisema.
Kinana alisema katika kushughulikia migogoro ya ardhi ni lazima wazungumze na Kamati za Ardhi ya Bunge ili isaidie.
MIKOA YENYE UKAME NA UPANDAJI MITI
ndugu mkuu wa mkoa nataka niombe hii mikoa ambayo inaukame ukame kidogo kwanini msitengeneze mkakati wa pamoja sijui kama mnao, mpande miti, unajua hii nchi ina bahati kubwa sana ya kuwa na kiongozi mmoja aliyekuwa mzuri sana .
Na kila jambo alikuwa vizuri, anaitwa Mwaliju Julius Nyerere kuna mradi hapa wengi wenu hamuujui kwasababu ya umri wenu ni mdogo, kuna ulikuwa unaitwa HASH ni mradi wa kupanda miti kwenye mikoa ya mwanza, Shinyangi na wakati huu Geita ,Simiyu kwasababu ya ukame , na fedha zikatafutwa nje na mwalimu nyerere alikuwa na kauli mbiu panda mti, kata mti .
Kwa hiyo mnatakiwa kupanda miti kama vichaa lakini ili mpande miti lazima muwe na mikakati, muwe na vitalu vya miti , lazima muwagawie wananchi wenu miti waweze kupanda sasa mimi ningeomba hii mikoa yenye ukame kuwe na mkakati wa pamoja mpange ma rc, mwite waziri wa misitu sijui kama waziri wa misitu anapanda miti au kazi yake ni kupambana na wananchi kwenye misitu, kazi ya waziri wa misitu namba iwe kupanda miti mwalimu alianzisha ule mradi na mwenyewe akawa mstari wa mbele.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akikagua jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na viongozi na Wana CCM baada ya kukagua jengo la Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akikagua jengo la Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifurahia wakati wa mkutano wa ndani wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani Geita.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wanachama wa CCM katika mkutano wa ndani akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).