Featured Kitaifa

BENKI YA NBC, KOLA PRODUCTS WATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA WA DON BOSCO

Written by mzalendoeditor
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mauzo wa Benki ya NBC Patrick Mashenene akifuatiwa na Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta
Na Mwandishi Wetu – Malunde 1 blog
 
Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC kwa kushirikiana na Kola Products wametoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wasalesia wa Don Bosco wanaotoka mikoa saba ya Tanzania.
 
Elimu hiyo imetolewa Jumanne Agosti 30,2022 wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga ambalo limehudhuriwa na vijana Wanaotoka mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Arusha , Kilimanjaro, Morogoro, Dar es Salaam na Iringa pamoja na wawakilishi kutoka Kenya ambako nyumba za Don Bosco zinapatikana.
 
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja amewaomba vijana hao kuchangamkia fursa ya mikopo yenye gharama nafuu kutoka kwenye benki yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuingiizia mapato serikali.
 
 
Naye Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta amewasihi vijana hao kuhakikisha wanakwenda kufanya kwa vitendo mafunzo ya ujasiriamali waliyopewa ili kuweza kujipatia kipato na hatimaye kuweza kuajiri watu wengine ili kutatua changamoto ya ajira.
 
Akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji, Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles amewasihi vijana hao wachangamkie fursa ya utengenezaji sabuni kwa sababu ni rahisi kuitengeneza, mtaji ni mdogo naa soko ni rahisi kupatikana.
 
Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Felix Wagi ameishukuru Benki ya NBC na Kola Products kwa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana hao.
 
 
Aidha amesema kongamano hilo hufanyika kila baada ya Miaka 2 kwa lengo la kuwaleta vijana hao wa madhehebu mbalimbali ya kikristo pia waislamu kuweza kujifunza mambo yanayohusu Maisha, wito, uchumi na hali ya Utandawazi.
 
 
“Kongamano hili ambalo mara zote hufanyika kwa siku tano, huratibiwa na kufadhiliwa na shirika la Don Bosco wakisaidiana na wadau mbalimbali pia michango ya ushiriki kutoka kwa vijana.Mwaka huu kongamano hili limefanyika mkoa wa Shinyanga katika shule ya Don Bosco Didia na kuhudhuriwa na Vijana 285 na walezi wao”, amesema Fr. Wagi.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Joyce Chagonja akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Meneja Biashara wa Benki ya NBC Fedrick Rutta akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga.
Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia Fr. Felix Wagi akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) lililofanyika katika shule ya Don Bosco Didia mkoani Shinyanga 
Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) likiendelea
Kongamano la Vijana wa Wasalesia wa Don Bosco (Salesian Youth Movement – SYM) likiendelea
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji.
Mkurugenzi wa Kola Products , Josephine Charles (kulia) akifundisha kwa vitendo juu ya utengenezaji wa sabuni za maji.
Vijana wakitengeneza sabuni za maji.
Vijana wakitengeneza sabuni za maji.

About the author

mzalendoeditor