Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU KUZINDUA MKAKATI WA KITAIFA WA UENDELEVU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGO’S)

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakili Amon Mpanju, akizungumza na Wadau mbalimbali wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua Mkutano wa kupitia Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, iliyofanyika Jijini Dodoma.

………………………………..

Na WMJJWM, Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatazamiwa kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwenye Jukwaa la mwaka la NGOs litakalofanyika jijini Dodoma Septemba 29 na 30, 2022.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kupitia rasimu ya Mkakati wa huo.
Wakili Mpanju amewataka Wadau kutoa maoni dhidi ya rasimu hiyo kwa ajili ya kupata Mkakati ambao utakuwa tayari kuzinduliwa na kutekelezwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
Ameongeza kuwa,  Kikosi Kazi kimekamilisha uchambuzi wa maoni yaliyopokelewa na tayari kimeandaa Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (National Strategy for NGOs Sustainability (NSNS).
“Kutokana na maoni mliyoyatoa imeweza kupatikana rasimu hii  ndio maana Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) ikaamua kufanya Mkutano huu wadau kwa ajili ya kuipitisha Rasimu hiyo.
Ninayo furaha kwamba tunayo rasimu ambayo baada ya maoni ya leo inafaa  kutoa muelekeo wa namna Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanaweza kuwa Endelevu hapa nchini, ” alisema Mpanju.
“Ni matumaini yangu mtashiriki kwa ukamilifu katika kutoa maoni chanya yatakayosaidia kuiboresha Rasimu iliyoandaliwa na Kikosi Kazi na  hatimaye kuwezesha utekelezaji wa Mkakati huo kwa ajili ya uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini na mustakabali wa Maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla” alisisitiza Mpanju.
Akitoa taarifa ya Kikosi kazi cha Uratibu wa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Bi. Nesia Mahenge amesema Kikosi Kazi hicho kimefanikiwa kupokea maoni kutoka kwa Wadau mbalimbali ndani ya Tanzania Bara na hivyo kufanikisha kupata rasimu ya Makakati huo muhimu kwa maendeleo ya NGOs na Taifa kwa ujumla.
“Tunawashukuru wadau kwa kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali unapatikana kwa Rasimu hii” alisema Nesia
Wadau mbalimbali wameshiriki kwenye hatua za kukamilisha mchakato wa uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NSNS). 
Kwa Mujibu wa taarifa hiyo Wadau walioshiriki kukamilisha ni pamoja na Timeless Business Solution,  Banki ya CRDB, PLC, KPMG East Africa  Tanzania Office, Stanbic Bank Tanzania (Mwanza), Amani Girls Home (AGH), PELUM Tanzania, CBM International and Aga Khan Foundation (Tanzania), Ubalozi wa Uingereza hapa nchini kupita Idara ya Foreign, Commonwealth and Development Office (FCDO) na Ubalozi Uswisi hapa nchini kupitia Idara yake ya Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC). 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakili Amon Mpanju, akizungumza na Wadau mbalimbali wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua Mkutano wa kupitia Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, iliyofanyika Jijini Dodoma 

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao akitoa maelezo ya Awali kuhusu mkutano wa Wadau kupitia rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, uliofanyika Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuandaa Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nesia Mahenge akitoa taarifa kuhusu Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, katika mkutano wa wadau uliofanyika Jijini Dodoma 

Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) Revocatus Sono akitoa salamu za Baraza hilo katika mkutano wa Wadau kupitia rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, uliofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma 

Baadhi ya Wadau walioshiriki kupitia rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, wakiwa katika mkutano huo uliofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju, akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua Mkutano wa kupitia Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa  Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, iliyofanyika leo Agosti 30,2022 Jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (WMJJWM)

About the author

mzalendoeditor