Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati akiwaaga Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI) katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma.
……………………….
Na Eva Godwin-DODOMA
UMOJA wa wanawake Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI) zaidi ya mia moja wameanza safari ya kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngorongoro lengo ikiwa ni kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya ndani vya utalii.
Akizungumza leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma wakati wa kuwaaga wanawake hao wa Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule amewataka watanzania kujenga utaratibu wa kutembelea vivutio vya utalii sambamba na kuelezea nia yake ya kuimarisha vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Mkoa wa Dodoma.
”Nawapongeza wanawake wa kanisa la aglikana kwa kujitoa kuunga juhudi za mh Rais Samia kwa kwenda Ngorongoro kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani hivyo niwaombe pia watanzania kujenga utaratibu kwa kutembelea vivutio vya utalii”.amesema
Amesema mapato ya nchi yanategemea na utalii, hivyo watumie fursa hii kuunga mkono juhudi za Rais kwani utalii ni fedha, utalii ni Burudani, Utalii ni uchumi .
Pia RC Senyamule amelisihi kanisa la Anglikana Mkoa wa Dodoma kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa maarifa na utashi wa kuliongoza taaifa la Tanzania.
Kwa upande wake Askofu wa Diocese ya Central Tanganyika (DCT), Dickson Chilongani amesema safari hiyo ya Wake wa Wachungaji na Maaskofu ni kwaajili ya Kuunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukuza na kutangaza utalii ndani na nje ya Nchi yetu pamoja na kwenda kufurahia mazingira ya ngorongoro.
“Tumeandaa kwa ajili ya kumuunga mkono Rais wetu kwa kuweza kukuza utalii katika Nchi yetu pamoja na kwenda kufurahia mazingira ya Morogoro, Ili watakapo rudi waendelee ma majukumu yao na Jumla ya Wake za Wachungaji na Maaskofu wanaokwenda Ngorongoro ni 100
” Hii ni awamu ya kwanza ambao wanakwenda lakini kuna awamu kama tatu kwasababu tuna Wake za Wachungaji pamoja na Maaskofu 300 na jitihada za Rais zitaendelea kuzaa matunda kupitia Utalii wetu”.Amesema Chilongani
Naye Katibu wa Umoja wa wanawake wake wa maaskofu Anglikana UWAKI askofu Agnes liheli ,amesema kuwa wazo hilo la kutembelea mbuga ya Ngorongoro lilikuwa la kimasiara lakini watu walilipokea vizuri bila kipingamizi na mikakati ya safari ilianza.
“Hili ni wazo ambalo kila mtu alilipitisha na moha kwa moja tukaliprleka kwa Baba askofu na muhitikio ulikuwa mkubwa japo kuna wengibe walisitasita na pia safari hii tumejiwezesha wenyewe japo na kanisa wametuchangia
” Sisi Wanawake wa Dayosisi hii tupo wengi ni zaidi ya 300 na tumeweka utaratibu tutakapo rudi tutaratibu safari nyingine na kila Mtu atakwenda na Tunatamani katika ziara hii tuwe mfano kwa Watu wengine kwasabau tunamuunga Mkono Rais wetu Samia Suluhu”. Amesema Liheli
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati akiwaaga Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI) katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma
Askofu wa Diocese ya Central Tanganyika (DCT), Dickson Chilongani,akizungumza mara baada Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,kuwaaga Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI) katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma
Katibu wa Umoja wa wanawake wake wa maaskofu Anglikana UWAKI askofu Agnes liheli,akizungumza mara baada Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,kuwaaga Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI) katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akiwa katika [icha mara baada ya kuwaaga Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI) katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma