KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga,akizungumza na Karani wa Sensa wakati alipokuwa akihesabiwa yeye pamoja na familia yake nyumbani kwake Kilimani jijini Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
……………………..
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga ameshiriki sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa yeye na familia yake nyumbani kwake eneo la Kilimani Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuhesabi Agosti 23,2022,Katibu Pili amewahimiza wakazi wa Dodoma kushiriki zoezi hilo kaa ukamilifu kwa kuandaa taarifa zao mapema ili hata wanapokuwa mbali na makazi yao waweze kuwaachia waliopo nyumbani.
“Sensa imeanza Agosti 23,2022,lakini zoezi litaendelea kwa siku saba,najua baada ya leo watu kupumzika,kesho wataendelea na majukumu yao hivyo andaeni taarifa ili kurahisisha uhesabiwaji,tukumbukuke sensa hii ni muhimu kwetu sisi sote na Taifa kwa ujumla,”amesema.