Featured Kitaifa

TULITAWALIWA KWA SABABU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA-WAZIRI MKENDA

Written by mzalendoeditor



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo juzi Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo juzi Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo juzi Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.
Mdau wa habari na elimu Bw Haki Ngowi akichangia mada wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari nchini na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda uliofanyika juzi Jijini Dar es salaam kutoa muelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo juzi Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari nchini mara badaa ya mkutano wake na wahariri kuelezea juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.
 

Na Mathias Canal, WEST-Dar es salaam

 

Katika
kutekeleza kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025
na mpango mkakati wa serikali kupitia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia mwaka 2022/2023
 imedhamiria kuwekeza zaidi kwenye Sayansi na Teknolojia ikiwa ni pamoja na eneo
muhimu la utafiti na elimu tiba.

 

Serikali
imeeleza kwa uwazi dhamira yake ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanavutiwa na
masomo ya Sayansi na Teknolojia ambapo imepanga kuwapatia udhamini wa masomo
kwa ngazi ya chuo kikuu kwa wanafunzi watakaofaulu vizuri matokeo ya kidato cha
sita katika masomo ya Sayansi na Elimu Tiba.

 

Pia katika
kuhamasisha uandishi katika majarida mbalimbali nchini serikali imepanga kutoa Shilingi
milioni hamsini kama motisha kwa wahadhiri kutoka chuo chochote cha serikali
ama binafsi watakaoweza kuchapisha andiko kwenye majarida ya juu.

 

Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo hivi
karibuni Jijini Dar es laam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari
nchini juu ya mwelekeo wa Wizara, Vipaumbele na maeneo ya kimkakati katika
utekelezaji kwa Mwaka wa fedha 2022/23.

 

Amesema kuwa
ili nchi iweze kuendelea inahitaji zaidi sekta ya Sayansi, Teknolojia na Tiba
kwani ndio msingi na moyo wa uchumi kwa taifa.

 

Amesema kuwa
mambo mengine yatafuata na yanapaswa kuendelea lakini ni wajibu wa serikali na
wadau wa elimu kuhakikisha kuwa Sayansi, Teknolojia na Elimu Tiba vinapewa
kipaumbele maradufu.

 

“Tulitawaliwa
kwa Sababu ya Sayansi na Teknolojia, Tulitumia Mishale na Mikuki wakaja na
Bunduki, Tulitumia ngalawa baharini wenyewe wanakuja na Mamerikebu makubwa ni
wazi tulitawaliwa kwa sababu hatukuwa na Sayansi na Teknolojia” Amekaririwa
Waziri Mkenda

 

Waziri
Mkenda amesema, pamoja na mambo mengine katika utoaji wa mikopo ya elimu ya
juu, serikali imeweka kipaumbele zaidi kwenye utoaji wa mikopo kwa wanafunzi
waliosoma masomo ya Sayansi, Uhandisi na Tiba.

 

Kuhusu
michango ya chakula shuleni, Prof Mkenda amesema kuwa ni kweli kuna muongozo wa
Lishe lakini zipo kaya zisizoweza kulipia kabisa kutokana na uduni wa maisha
hivyo serikali inaliangalia na kulifanyia kazi jambo hilo.

About the author

mzalendoeditor