MSANII wa filamu mkongwe na mtangazaji, Chuma Suleiman almaarufu Bi Hindu, amefariki dunia asubuhi hii, nyumbani kwake, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa mkongwe huo huku sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni maradhi ya muda mrefu.