Featured Kitaifa

TAKUKURU MIKOA ZATAKIWA KUIMARISHA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA MASHULENI ILI KUJENGA JAMII YENYE MAADILI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa usimamizi wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora bi. Leila Mavika akizungumza wakati akihitimisha  fainali ya mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tukio lililofanyika leo Julai 2,2022 katika shule ya Sekondari Maria De Mathias.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwango  akizungumza wakati kuhitimisha  fainali ya mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tukio lililofanyika leo Julai 2,2022 jijini Dodoma katika shule ya Sekondari Maria De Mathias.

Mkurugenzi wa usimamizi wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora bi. Leila Mavika wa pili kutoka kushoto akimkabidhi tuzo ya ushindi mwakilishi wa wanafunzi kutoka shule ya sekondari Maria De Mathias Jasmini Ibrahimu mara baada ya kuibuka washindi kwenye shindano hilo.

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule 6 zilizoingia fainali ya mashindano hayo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitokea wakati fainali ya mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tukio lililofanyika leo Julai 2,2022 jijini Dodoma katika shule ya Sekondari Maria De Mathias.

Mkurugenzi wa usimamizi wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora bi. Leila Mavika kwanza kutoka kushoto akiwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo wakifuatilia mdahalo kwa wanafunzi (hawapo pichani) wakati fainali ya mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tukio lililofanyika leo Julai 2,2022 jijini Dodoma katika shule ya Sekondari Maria De Mathias.

Baadhi ya wanafunzi wakitoa burudani wakatiwa wa  kuhitimisha  fainali ya mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tukio lililofanyika leo Julai 2,2022 jijini Dodoma katika shule ya Sekondari Maria De Mathias.

Mkurugenzi wa usimamizi wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora bi. Leila Mavika aliyekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walioshiriki mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha TAKUKURU Mkoa wa Dodoma tukio lililofanyika leo Julai 2,2022 jijini Dodoma katika shule ya Sekondari Maria De Mathias.

……………………………………..

Na  Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU za Mikoa zimetakiwa kuanzisha na kuzimarisha klabu za wapinga rushwa za wanafunzi mashuleni na kuzipa mafunzo ya jinsi ya kuzuia na kupambana na rushwa  ili kujenga jamii ijayo itakayokuwa na maadili na kuchukia vitendo vya rushwa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa usimamizi wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Leila Mavika wakati wa fainali ya mashindano la mdahalo kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwa wanachama wa klabu  za wapinga rushwa za shule za sekondari za Jiji la Dodoma.

Ambapo amesema kuna haja ya kuziimarisha klabu za wanafunzi wapinga rushwa ili kuimarisha maadili katika jamii ambayo itakuwa inachukia vitendo vya rushwa.

“Kwenye utumishi wa umma kitachohitajika ni utaalmu, uaminifu na uwajibikaji na ninaamini kuwa endapo tutaimarisha klabu za wapinga rushwa utaweza kupata watumishi wa umma wa baadaye watakaokuwa na hivi vigezo” amesema bi. Leila.

Amesema ni lazima kila mwananchi awe mzalendo kwa nchi yake kwa kupinga vitendo vya rushwa hivyo ninaamini kama tutaimarisha tangu utotoni tutafanikiwa kijenga kizazi chenye maadili.

Ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Dodoma kwa kuja na ubunifu wa mashindano hayo ambayo amesema yatawaimarisha wanafunzi katika kivichukia vitendo vya rushwa na kupata viongozi waadilifu wa baadaye.

Awali Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma  Sosthenes Kibwengo amesema mashindano hayo yalianza mwezi wa 4, 2022 yakishirikisha shule za sekondari 58 na zilikuwa zikipungua na hatimae shule 6 kuingia fainali.

Amesema maada katika mdahalo huo ilikuwa ni udhibiti wa vitendo vya rushwa katika miradi ya maendeleo maada ambayo ililenga kuwajengea uwezo wanafunzi na jamii katika kusimamia miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao.

“Fedha zinazotumika katika miradi ya maendeleo ni kodi za wananchi kwahiyo tunalenga kupitia mashindano hayo tunawajengea uwezo wanafunzi kutambua na kuwa nauelewa katika kudhibiti vitendo vya rushwa kwenye miradi.

Tunaamini kuwajengea uwezo watoto hawa watakwenda kutoa elimu katika maeneo yao na watakwenda kuelemisha jamii zinazowazunguka kupata uelewa wa kudhibiti vitendo vya rushwa katika miradi na usimamizi wa miradi hiyo” Amesema Kibwengo.

Amesema mashindano hayo yalilenga kuwajenga vijana katika mapambano dhidi ya rushwa ili kuwa na jamii ambayo inaichukia rushwa na watumishi wa umma wa maadaye wenye maadili kwenye utumishi wao.

“Tunaamini kupitia mafunzo haya wanafunzi hao watakwenda kuwa mabalozi wa zuri kwenye familia zao na taifa kwa ujumla na tutakuwa tumebadilisha jamii kwa kiasi kikubwa” amesema.

Shule 6 zilizoingia fainali ni Shule ya Sekondari Maria De Mathias, Bunge High School, Makutopora, Chinangali, Dodoma Sekondari na Itega Sekondari huku shule ya Sekondari Maria De Mathias wakiibuka washindi na kupata zawadi ya shilingi laki tatu.

About the author

mzalendoeditor