Featured Kitaifa

WAZIRI NDUMBARO AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI UJENZI JENGO LA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi huo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30, 2022.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro,akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa  Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo  katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30, 2022.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro,akitoa maelezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa  Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo  katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30, 2022.

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro,aakizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30, 2022.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geofrey Pinda,akizungumza mara baada ya Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro,kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30, 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,Mary Makondo,akimshukuru Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro kwa kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30,

Katibu wa Kikosi Kazi cha  Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa mji wa Serikali  Bw.Meshack  Bandawe,akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30,

 Mhandisi Nassiri Nassoro kutoka SUMA JKT,akitoa taarifa ya mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Katiba na Sheria kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30,

MUONEKANO wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Katiba na Sheria ukiendelea

……………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro, amemtaka Mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT anayetekeleza Mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara hiyo kuongeza kasi ya ujenzi ili likamilike kwa wakati.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 30, 2022.

Dk.Ndumbaro, ameonesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo. Amemtaka mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT kuongeza kasi ya ujenzi ili likamilike na hatimaye lianze kutumika.

“Pamoja na kuwa mradi huu tunatakiwa tuukamilishe kwa wakati lakini ikiwezekana hata ukamilike mapema zaidi.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Mhandisi Nassiri Nassoro kutoka SUMA JKT amesema kuwa kazi mbalimbali zinaendelea kutekelezwa kulingana na mpango kazi (master program) uliowekwa.

Mhandisi Nassoro ameongeza kuwa hadi kufikia sasa mkandarasi ameshakamilisha kazi ya ujenzi wa mradi kwa asilimia 33 na kuwa wana matumaini ya utakamilika kwa wakati.

Hata hivyo, amesema kuwa anakabiliwa na changamoto ya kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi vikiwemo nondo.

About the author

mzalendoeditor