Watu 16 wakiwemo wageni walijeruhiwa nchini Saudi Arabia wakati ufalme huo ulipoharibu ndege isiyotumia rubani-DRONE iliyorushwa dhidi ya uwanja wa ndege wa waasi wa Yemen, ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia ulisema Jumatatu.
Ni shambulizi la pili katika uwanja wa ndege kwenye kipindi cha chini ya wiki mbili linalodaiwa kufanywa na waasi wa ki-Houthi wanaoungwa mkono na Iran. Waasi hao mara kwa mara hufanya mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia ambayo kwa miaka saba imeongoza muungano wa kijeshi ambao uliingilia kati kuiunga mkono serikali ya yemen katika kukabiliana na matendo ya wa-Houthi.
Ndege isiyotumia rubani iliyorushwa kuelekea uwanja wa ndege wa Mfalme Abdullah huko Jazan, iliharibiwa na vipande vyake vilianguka ndani ya uwanja huo, muungano huo ulisema, kama ilivyoripotiwa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia. Raia 16 wa mataifa tofauti walijeruhiwa ilisema taarifa ikiwashutumu wa-Houthi kwa kuanzisha tena mashambulizi ya kuvuka mpaka kutoka uwanja wa ndege wa Sanaa.
CHANZO:VOASWAHILI