Kizimkazi, Zanzibar
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, ambaye pia ni Mbunge anayewakilisha Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Mbeya, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, leo Septemba 8, 2026, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani kwake Kizimkazi, Zanzibar, na kumpa pole kufuatia kifo cha Mwenza wake, Mzee Hafidh Ameir Hassan.
Mhe. Maryprisca amemfariji Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo, huku akitoa pole na kuwaombea moyo wa subira, uvumilivu na faraja katika kipindi hiki cha majonzi.
Mzee Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mzena na amezikwa siku hiyo hiyo Visiwani Zanzibar.