Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Mchafu akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na Taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira, wakati wakikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.
Na: OWM (KAM), Dodoma
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kuhakikisha kuwa ajira zinazozalishwa nchini pamoja na fursa za ajira za nje ya nchi zinakuwa za staha na zenye tija ili kuwawezesha Watanzania kufanya kazi zinazokidhi viwango, usalama wa haki zao na kuwalinda dhidi ya mazingira hatarishi.
Amesema hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Chakoma Mchafu, leo Agosti 13, 2026, Jijini Dodoma wakati kamati hiyo ikipokea taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira.
Akizungumza mara baada ya kupokea na kujadili taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mchafu, amesisitiza kuwa mafanikio ya ajira nchini hayapaswi kupimwa kwa kuangalia idadi ya nafasi za ajira zilizotangazwa au idadi ya waliounganishwa na fursa hizo za ajira pekee. Amesema, kipimo kikubwa kinapaswa kuwa ni idadi ya Watanzania waliopata ajira za staha na zenye tija ili kuwawezesha watanzania kufanyakazi zinazokidhi viwango, usalama wa haki zao na kuwalinda dhidi ya Mazingira hatarishi.
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo imepongeza fisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kwa hatua mbalimbali inazochukua katika kushughulikia masuala ya ajira, hususani kwa vijana, ikiwemo kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuongeza fursa za ajira zenye ubora na zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Ofisi hiyo itaendelea kuwaunganisha watafutakazi na fursa mbalimbali za ajira ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Mchafu akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na Taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira, wakati wakikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii mara baada ya kuwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na Taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mary Maganga akiwasilisha taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakichangia hoja mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na Taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akieleza jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo wa WCF, katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2025/2026, katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2025/2026, pamoja na Taarifa ya Uratibu wa zoezi la Utambuzi, Usajili na Upangaji wa Maeneo ya Kazi kwa Watafuta Kazi; Mchakato wa Uratibu Upatikanaji na Usimamizi wa Ajira za Nje ya Nchi; na Udhibiti na Usimamizi wa Vyombo vya Ajira na Ukusanyaji wa Taarifa za Soko la Ajira wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 13 Agosti, 2026.