Featured Kitaifa

KATIBU NENELWA MWIHAMBI ATETA NA MKURUGENZI WA MASUALA YA KIMATAIFA KUTOKA BUNGE LA CAMEROON

Written by mzalendoeditor

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa kutoka Bunge la Cameroon, Ndg. Oliver Tiengeya Moh (katikati) alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akiangalia bahasha yenye Ujumbe Maalum kutoka kwa Spika wa Bunge la Cameroon, Mhe. Cavaye Yeguie Djibril uliowasilishwa na  Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa kutoka Bunge la Cameroon, Ndg. Oliver Tiengeya Moh (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa kutoka Bunge la Cameroon, Ndg. Oliver Tiengeya Moh (wapili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo na Mshauri wa Masuala ya Kisheria Ofisi ya Bunge, Ndg. Thomas Shawa

(PICHA na PATSON SOBHA – OFISI YA BUNGE)

About the author

mzalendoeditor