Featured Kitaifa

RUWASA WILAYA YA GEITA YA SAINI MKATABA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA VIREFU 8

Written by mzalendoeditor

Na.Costantine James, Geita.

Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Geita imetiliana saini Mkataba wa kuchimba visima na Kampuni ya Intra Resources wenye thamani ya milioni 217.

Utiaji saini wa makataba huo Kati ya Ruwasa Wilaya ya Geita na Kampuni ya Intra Resources kutoka jijini Dar es Salaam umefanyika Leo tarehe 17 juni 2022 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Geita.

Mradi huo utakao husisha uchimbaji wa visima 8 wilayani Geita Utaghalimu kiasi cha milioni 217 unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu hali itakayosaidia kuongeza kwa upatikanaji wa maji ndani ya wilaya ya Geita.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa amesema mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kuhudumia watu 3250 ndani ya wilaya ya Geita kwa kupata maji safi na salama.

Mhandisi sande amesema mkataba huo unamtaka mkandarasi aliepewa dhabuni hiyo kuhakikisha anakabidhi kisima cha maji chenye kutoa maji lita elfu tatu kwa sasa tofauti na hapo kitakua kimeharibika na ni Mali ya Mkandarasi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Intra Resources Limited Mikidadi Mohamed Amesema atahakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha uchimbaji wa visima hivyo 8 unakamilika kabla ya mda uliopangwa.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amesema utiliaji saini wa mkataba huo ndani ya mkoa wa Geita unaenda kuongeza idadi ya visima vitakavyochibwa ndani ya mkoa kwa lengo la kuongeza hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Amesema Mkoa wa geita unatekeleza uchimbaji wa visima 33 vinavyo ghalimu milioni 800 kwa visima vyote na pindi miradi hiyo itakapokamilika itawezesha wananchi 160,000 kupata huduma ya maji safi na salama katika mkoa wa Geita .

Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe, Wilson Shimo amesema mradi huo unakwenda kutatua kero ya maji ndani ya wilaya ya Geita amemutaka mkandarasi alieshinda dhabuni hiyo kuhakikisha anakamilisha kwa wakati ili wananchi waanze kupata maji.

Mhe, Shimo amewataka wananchi ndani ya wilaya ya Geita ambapo visima hivyo vitachibwa kuhakikisha wanatunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa mda mrefu kwani serikali imedhamilia kuwasogezea wananchi huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao.

About the author

mzalendoeditor