Na. Veronica Mwafisi-Tabora
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaambia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora kuishi katika maadili wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza shule ili wajiepusha na tabia ambazo zitawafanya wajiingize katika makundi yasiyofaa ya uvunjivu wa amani.
Mhe. Ridhiwani amesema hayo leo tarehe 11 Julai, 2026 alipotembelea shule hiyo kabla ya kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu mkoani humo.
Amesema kuna maisha baada ya kumaliza shule, hivyo wanafunzi hao wanatakiwa wakawe mfano mzuri katika maadili na uzalendo kwa wengine huko wanakoenda kutokana na sifa za shule hiyo.
“Shule hii imetoa viongozi wengi sana, waadilifu na wazalendo, hivyo mtunze heshima yake, mkajitofautishe na wengine, msiige tabia ambazo sio nzuri,” amesisitiza.
Amepongeza uongozi wa shule hiyo kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka huu na miaka iliyopita na ufaulu mzuri pia hata kwa kidado cha nne na kuwasihi kuendelea kufanya vizuri zaidi ili elimu hiyo iwakomboe wao binafsi na taifa kwa ujumla.
Aidha, ametoa wito kwa Viongozi wa Mkoa wa Tabora kuwa karibu na wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine zote ili wawasaidie kukua kimaadili.
“Watoto hawa ni wadogo, tuwasaidie hata watakapotoka hapa waendelee kuwa na sifa nzuri huko watakakokwenda.
