Featured Kitaifa

MILIONI 80 ZA MBUNGE VITI MAALUM ARUSHA ZASUBIRI MIRADI ILI KUNUFAISHA WANAWAKE

Written by mzalendoeditor

Mbunge viti maalum mkoa wa Arusha Zaytun Swai akiwasilisha taarifa katika baraza la UWT mkoa wa Arusha ya mambo aliyoyatekeleza tangu uchanguzi 2020 Hadi 2021 ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ilani ya CCM.

Mbunge Zaytun Swai akiwa pamoja na wanawake wa umoja wa UWT mkoa wa Arusha wakionyesha kitabu cha mambo aliyoyafanya mbunge huyo pamoja na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

…………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Zaytun Swai amesema kuwa ahadi ya mpango wa kutoa ufadhili wa miradi yenye thamani ya shilingi milioni 80 aliyotoa Januari 16 mwaka huu kwaajili ya kuwawezesha wanawake wa mkoa wa Arusha  bado ataitimiza anachosubiri ni miradi kutoka katika wilaya.
Mbunge Zaytun aliyasema hayo katika kikakoa cha baraza la umoja wa wanawake mkoa wa Arusha ambapo alieleza kuwa ili kuhakikisha miradi yote itakayotokana na fedha hizo inakuwa endelevu aliandika barua kwa mwenyekiti wa UWT taifa kwa lengo kutoa taarifa kwa kwa viongozi wa UWT mkoa na katika ngazi za wilaya kuandaa miradi itayopokea fedha hizo.
“Mpaka hivi Sasa sijapokea miradi yoyote ofisini kwangu ili nianze kutimiza ahadi hii muhimu sana kwa maendeleo ya wanawake lakini niwaondoe shaka kwamba ahadi hii itatimizwa kama nilivyoahidi ninachosubiri ni miradi,” Alisema Zaytun.
Aidha kwa upande wa mafanikio ya utekelezaji wa ilani alisema kuwa amefanikiwa kuhamasisha shughuli za maendeleo ya mkoa wa Arusha ndani na nje ya chama, kuwezeha kufanyika kwa ya UWT wilaya mbalimbali, kusaidia chama kusimamia miradi ya serikali kwa kutembelea miradi mbalimbali katika wilaya pamoja na  kuhamasisha viongozi wa UWT kusajili wanachama wapya  ili kuongeza wanachama wa chama cha mapinduzi.
“Lakini pia nimweza kushirikiana katika kugharamia huduma za jamii kama vile kutafuta madawati na vifaa tiba kwaajili ya shule na hosipitali za mkoa wa Arusha na kubwa zaidi ni nimeweza kushiriki katika shughuli za kijamii lengo likiwa ni kukiweka chama karibu na wananchi,” Alisema.
Alifafanua kuwa kwa miaka iliyobaki anatarajia kuendelea kushughulikia wezeshaji wananchi kiuchumi kwa kuendelea kutafuta fursa pamoja na kusimamia halmashauri zote saba kuhakikisha zinatenga asilima 10 kwaajili ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu pamoja na kuhakikisha bajeti inayotengwa na serikali kwaajili ya mkoa wa Arusha hasa ya miradi ya maendeleo, inatolewa.
“Nitaendelea kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa nyumba za viongozi wa UWT katika wilaya za mkoa wa Arusha na katika sekta ya huduma Kuna maeneo bado yana mahitaji makubwa ya maji, miundombinu ya Elimu, afya na barabara, nitaendelea kuwasilisha changamoto hizi serikalini ili kuhakikisha zinapata ufumbuzi,” Alieleza.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa ataendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo zikiwemo ofisi za  balozi, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na za umma ili kutafuta rasilimali fedha kwaajili ya kutatua changamoto mbalimbali za afya, maji na elimu.

About the author

mzalendoeditor