Featured Kitaifa

SERIKALI YAONGEZA NGUVU KATIKA KUWAINUA VIJANA BALEHE BAADA YA TATHMINI YA NAIA

Written by Alex Sonna

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa kupokea matokeo ya tathmini ya mwisho ya utekelezaji wa ajenda ya kitaifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo ya vijana balehe (NAIA) uliofanyika leo Aprili 23,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wasikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa kupokea matokeo ya tathmini ya mwisho ya utekelezaji wa ajenda ya kitaifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo ya vijana balehe (NAIA) uliofanyika leo Aprili 23,2026 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  Mkutano wa wadau wa kupokea matokeo ya tathmini ya mwisho ya utekelezaji wa ajenda ya kitaifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo ya vijana balehe (NAIA) uliofanyika leo Aprili 23,2026 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-DODOMA

SERIKALI imeanza kufungua ukurasa mpya wa uwekezaji kwa vijana baada ya kupokea matokeo ya tathmini ya ajenda ya maendeleo ya vijana balehe, hatua inayolenga kuimarisha mikakati ya kuwawezesha vijana kukabiliana na changamoto na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Akifungua mkutano huo uliofanyika leo Aprili 23,2026  jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, amesema tathmini hiyo ni nyenzo muhimu ya kupima hatua iliyofikiwa na kupanga mikakati madhubuti ya kusonga mbele.

Amesema tangu kuanzishwa kwa ajenda hiyo, mafanikio kadhaa yamepatikana, ikiwemo kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana, uelewa mpana wa elimu ya uzazi na ongezeko la programu za kuwawezesha vijana kujiajiri. Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza kasi ili kuhakikisha huduma hizo zinawafikia vijana wote bila ubaguzi.

“Tumetoka mbali, lakini hii si mwisho. Ni mwanzo wa hatua mpya ya kujiuliza tunakwenda wapi na kwa kasi gani,” amesema Mpanju.

Ameeleza kuwa ajenda hiyo imelenga kushughulikia changamoto zinazoathiri moja kwa moja ustawi wa vijana balehe, zikiwemo maambukizi ya VVU, mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia, lishe duni, utoro shuleni pamoja na ukosefu wa ujuzi wa kujiajiri.

Kwa mujibu wa tathmini hiyo, uwekezaji sahihi katika sekta za afya, elimu na ustawi wa jamii umeonesha matokeo chanya katika kubadili maisha ya vijana wengi. Hata hivyo, bado kuna pengo katika upatikanaji wa huduma hizo hususan katika maeneo ya vijijini na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.

Mpanju amewataka wadau kutumia matokeo ya tathmini hiyo kama dira ya kubaini maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi na kuweka mikakati itakayohakikisha hakuna kijana anayebaki nyuma.

“Tusibaki kwenye takwimu pekee, bali tuzitafsiri katika mabadiliko halisi ya maisha ya vijana wetu,” amesisitiza.

Ametaja miradi ya AHADI, BRIGHT na VUMA kuwa miongoni mwa mipango iliyochangia mafanikio hayo, kwa kusaidia kupanua wigo wa huduma rafiki za afya, kutoa elimu ya uzazi na kuwajengea vijana ujuzi wa maisha na kujitegemea kiuchumi.

Aidha, amepongeza mchango wa washirika wa maendeleo, hususan mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na taasisi zisizo za kiserikali, kwa ushirikiano wao wa karibu katika kufanikisha utekelezaji wa ajenda hiyo pamoja na tathmini yake.

Pia Mpanju amesisitiza umuhimu wa ubunifu na mawazo mapya katika kuboresha programu za vijana, akieleza kuwa mazingira yanayobadilika yanahitaji mbinu mpya za kufikia malengo yaliyokusudiwa.

“Vijana wa leo ndio watakaoamua sura ya Tanzania ya kesho. Ni jukumu letu kuwaandaa sasa kwa kuwapa maarifa, ujuzi na fursa zinazohitajika,” amesema.

Kwa upande wake, Dkt. Ahmad Mukuwani, aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, amesema Ajenda ya Taifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (NAIA) imekuwa na mchango mkubwa katika kuwahamasisha vijana wengi kujiunga na vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) ili kupata ujuzi unaowawezesha kujitegemea na kuchangia ukuaji wa uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa hata miongozo ya Wizara ya Elimu imeendelea kusisitiza umuhimu wa lishe shuleni, ambapo kwa sasa shule nyingi zimeanza kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi, hatua inayochangia kuboresha afya na uwezo wao wa kujifunza.

Hata hivyo, Dkt. Mukuwani amebainisha kuwa pamoja na mafanikio hayo, bado zipo changamoto zinazoendelea kuwakabili vijana, ikiwemo maambukizi ya VVU, mimba za utotoni na ndoa za utotoni.

“Pamoja na mafanikio ya ajenda hii, bado kuna changamoto za VVU, mimba za utotoni na ndoa za utotoni. Hivyo, kuna haja ya kuendelea kuwekeza zaidi ili kuhakikisha watoto wetu wanaepukana na changamoto hizo,” amesema.

Matokeo ya mkutano huo yatachangia kuimarisha mikakati ya maendeleo jumuishi nchini, na hatimaye kusaidia kujenga kizazi cha vijana chenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo huku kikichangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

About the author

Alex Sonna