Featured Kitaifa

RAIS DKT. SAMIA AZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA

Written by Alex Sonna

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, funguo mara baada ya kuzindua jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Na.Alex Sonna,Mzalendo blog-KIKOMBO DODOMA

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuliwezesha Jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuhakikisha usalama wa raia na Taifa unaimarika zaidi.

Akizungumza leo Februari 24,2026 jijini Dodoma katika hafla ya ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa kikombo Rais Samia, amesema kuwa kila hatua ya maendeleo iliyofikiwa nchini imejengwa katika misingi ya utulivu, nidhamu na ulinzi thabiti kwa wananchi wake.

Amesisitiza kuwa bila amani na usalama wa kutosha, shughuli za kiuchumi na kijamii haziwezi kustawi kwa kiwango kinachotarajiwa.

 “Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuimarisha miundombinu ya kijeshi, kuongeza vitendea kazi pamoja na kuboresha maslahi ya wanajeshi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uzalendo mkubwa. ameongeza kuwa uwekezaji katika sekta ya ulinzi si tu kulinda mipaka ya nchi bali pia kulinda rasilimali, watu na mustakabali wa taifa kwa ujumla.”amesema Mhe Dkt.Samia

kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT ,Dkt .Rhimo  Nyansaho amesema ujenzi wa makao makuu hayo unaonesha dhamira ya wazi ya serikali katika kuimarisha suala la ulinzi na usalama nchini.

Amesema jengo hilo la kisasa litaongeza ufanisi katika uratibu wa shughuli za kiulinzi na kutoa mazingira bora ya utendaji kazi kwa maafisa na askari.

“Uwepo wa makao makuu ya kudumu ni hatua muhimu katika kujenga taasisi imara, zenye mifumo madhubuti ya kiutendaji na mawasiliano, jambo litakalosaidia kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazoibuka katika ulimwengu wa sasa.”amesema Dkt.Nyansaho

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Faraji Mnyepe amesema serikali imeandika historia mpya kwa kuwa na makao makuu ya kudumu ya ulinzi wa taifa.

Amesema zaidi ya shilingi bilioni 121 zimetumika katika kufanikisha ujenzi huo ambao umetekelezwa na wataalamu wa ndani ya jeshi hilo.

“Matumizi ya wataalamu wa ndani yamepunguza gharama na kuongeza uzoefu kwa wanajeshi katika sekta ya ujenzi na usimamizi wa miradi mikubwa ya kimkakati. ameongeza kuwa mradi huo umezingatia viwango vya kisasa vya ubora na usalama.”amesema Dkt.Mnyepe

Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Tanzania, Jenerali Jacob Mkunda amesema jengo hilo ni sehemu ya kurahisisha utendaji kazi na kuchochea uimarikaji wa ulinzi na usalama wa taifa. amesema makao makuu hayo yatawezesha upangaji na utekelezaji wa mikakati ya kiulinzi kufanyika kwa haraka na ufanisi zaidi.

Aidha amewahimiza wanajeshi kuendelea kufanya kazi kwa nidhamu, uadilifu na uzalendo, wakitambua kuwa jukumu lao ni kulinda uhuru, umoja na mshikamano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipiga light pistol juu kuashiria uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi bendera Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, funguo mara baada ya kuzindua jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maafisa Askari, Watumishi wa umma na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

Matukio mbalimbali katika uzinduzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026.

          

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma tarehe 24 Februari, 2026

About the author

Alex Sonna