Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI MASANJA AELEKEZA KUJENGWA KITUO KUKABILIANA NA TATIZO LA TEMBO NACHINGWEA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Namapuya wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu tembo kuvamia makazi ya watu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu tembo kuvamia makazi ya watu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo.

Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mhe. Dkt. Amandus Chinguile akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)  ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu tembo kuvamia makazi ya watu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimpa mkono wa pole mjomba wa familia ya marehemu Riziki Issa, Musa Bakari baada ya kijana huyo kuuawa na tembo katika kijiji cha Namanja Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.

Mkazi wa Kijiji cha Namapuya Juma Stambuli akielezea namna tembo ilivyoathiri wananchi, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)  ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu tembo kuvamia makazi ya watu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo

Mkazi wa Kijiji cha Namanja Binasa Tingo akielezea namna tembo ilivyoathiri wananchi, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)  ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu tembo kuvamia makazi ya watu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo.

Baadhi ya Askari wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi  ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu tembo kuvamia makazi ya watu Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi leo.

**************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameelekeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kujenga kituo cha askari wa uhifadhi katika kijiji cha Namapuya na Namanja Wilayani Nachingwea ili kukabiliana na changamoto ya tembo wanaovamia makazi ya watu wakitokea Pori la Akiba Selous.

Ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi kuhusu changamoto za tembo wanaovamia makazi ya watu katika vijiji vya Namapuya na Namanja Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.

Aidha, ameelekeza kuwekwe mizinga ya nyuki katika shoroba ambazo tembo hao wanapita ili kuzuia wasifikie makazi ya watu.

Mhe. Masanja amewaasa wakazi wa maeneo hayo kuacha fikra za kutaka kuua tembo kwa sababu mnyama huyo analindwa na sheria za Kimataifa.

“Mkakati wa Serikali ni kuangalia namna wananchi wanaoathirika na tembo wanaweza kunufaika na rasilimali ya mnyama huyo kwa kuunda mfuko maalum” Mhe. Masanja amefafanua.

Katika ziara hiyo, Mhe. Masanja alitembelea familia iliyoathirika na tembo na kutoa mkono wa pole ambapo kijana wa familia hiyo, Riziki Issa aliuawa na tembo akiwa katika majukumu yake.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mhe. Dkt. Amandus Chinguile ameishukuru Serikali kwa kuchukua hatua ya kutembelea eneo hilo lenye changamoto ya kuvamiwa na wanyama wakali na waharibifu kama tembo.

Awali, Mkazi wa Kijiji cha Namanja Binasa Tingo alitoa malalamiko kwamba kutokana na tembo kuingia kwenye makazi ya watu, wanashindwa kuendelea na shughuli za kila siku za shamba, kuchota maji n.k.

Mkazi wa Kijiji cha Namapuya, sais Ngololo ameongeza kuwa kufuatia tatizo la tembo kijijini hapo wananchi wamekuwa wakiishi kwa shida kwa kukoa chakula baada ya tembo kula mazao yao mashambani

About the author

mzalendoeditor