Featured Kitaifa

WAHITIMU CHUO CHA USTAWI WA JAMII WATAKIWA KUBADILI HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KUWA BIASHARA

Written by Alex Sonna

 

Na Mwandishi Wetu, 

Wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) wametakiwa kuwa wabunifu na kubadilisha elimu ya huduma za ustawi kuwa biashara ili kujiajira wenyewe huku lengo kuu ni kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii zao.

Akizungumza katika Mahafali ya 49 ya Chuo  cha Ustawi wa Jamii Kampasi ya Dar Es Salaam na Mahafali ya nane ya Kampasi ya Kisangara kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Mkuu wa Wilaya Temeke, Sixtus Mapunda amewaasa kuitumikia taifa kwa utii na uadilifu.

“Mkawe wabunifu mkajiongeze dunia imebadilika mahitaji ya wananchi ni mengi 

 

Elimu ya saikolojia haikuwa biashara kwasasa inahitajika sana katika jamii zetu na mnapata fedha hivyo tuhamishie huduma za ustawi wa jamii kuwa biashara kuna makampuni na taasisi wanahitaji huduma hizi tuwe na juhudi na kuna matokeo ya juhudi za muda mrefu,” amesisitiza Mhe. Mapunda

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema wahitimu hao katika fani mbalimbali za huduma za ustawi wa jamii watatumika kuisaidia jamii kutatua changamoto zao katika kuleta Ustawi wao.

Naye Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dk Joyce Nyoni amesema kwa mwaka wa masomo 2025/2026 Chuo kimeanzisha programu mpya nne ikiwemo masomo na maendeleo ya ujasiriamali, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, kazi za jamii, watoto na vijana na mafunzo ya makuzi na malezi ya awali kwa watoto.

Amesema katika mahafali hayo kuna jumla ya wahitimu 3100 kati yao 2017 ni wanawake na wanaume ni 1083 walitunukiwa tuzo zao katika fani mbalimbali za ustawi wa jamii.

 

 

 

 

 

About the author

Alex Sonna