Featured Kitaifa

TANZANIA NA SAUDI ARABIA KUONGEZA FURSA ZA ELIMU

Written by Alex Sonna

 

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amekutana na Balozi wa Falme za Kiarabu Saudi Arabia, Mhe. Yahya Bin Ahmed Okeish, ambapo wamejadili kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu pamoja na kuongeza fursa za skolashipu kwa vijana.

Prof. Mkenda ameishukuru Saudi Arabia kwa kuongeza nafasi za ufadhili masomo ya jelimu ya juu kutoka 90 hadi 127 kwa wanafunzi wa watanzania, na ameahidi kuwa Serikali itazitumia kikamilifu fursa hizo ili kuwawezesha vijana kupata elimu chini humo.

Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vijana wanapata elimu stahiki katika maeneo ya kimkakati, ikiwemo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Sayansi ya Takwimi na Akili Unde.

Kwa upande wake, Mhe. Okeish amesema Saudi Arabia inajivunia ushirikiano wake na Tanzania katika sekta ya elimu na itaendeleza ushirikiano huo katika kutekeleza mikakati ya kuendeleza elimu na ujuzi kwa vijana wa Kitanzania kulingana na vipaumbele vya taifa.

Aidha, ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuwa na Sera Bora ya Elimu na pia mipango yake ya kufanya ziara nchini Saudi Arabia kutembelea vyuo mbalimbali, kubadilisha a uzoefu na kupanua fursa za elimu kwa vijana wa mataifa yote mawili ikiwemo suala la kuimarisha ufundshaji lugha ya kiarabu.

About the author

Alex Sonna