Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukua hatua za kimkakati kuhakikisha changamoto zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu nchini zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Akizungumza leo tarehe 03 Desemba, 2025 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akipiga picha pamoja na watu wenye ulemavu kwenye hafla iliofanyika leo tarehe 03 Desemba, 2025 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akikabidhi mashine ya kusagia nafaka kwa kikundi cha watu wenye ulemavu cha Kizimkazi Mkunguni.
“(Pichani) Jackline Bakari Mtaita, muimbaji wa kizazi kipya kutoka Sawa Organization, akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, baada ya kuimba wimbo wake kuhusu watu wenye ulemavu, katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Watu Wenye Ulemavu leo tarehe 03 Desemba, 2025 atika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja,
(PICHA NA IKULU ZANZIBAR)
Ahmed Abdul-shakur Abdalla