Kundi kubwa la watalii 261 wametua leo tarehe 02 Desemba 2025 Hifadhi ya Taifa Mikumi wakitokea Zanzibar kushuhudia uzuri wa Hufadhi hiyo ya kipekee.
Kupitia urahisi wa usafiri kati ya Zanzibar na Hifadhi ya Taifa Mikumi wageni hawa wamepata fursa ya kuingia moja kwa moja hifadhini na kuanza kuona wanyamapori ndani ya muda mfupi tu baada ya kutua.
Hifadhi ya Taifa Mikumi inazidi kuwa kitovu cha utalii wa safari, ikitoa mchanganyiko mahsusi wa urahisi wa kufika na uzoefu wa karibu na wanyamapori katika makazi yao ya asili.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miundombinu ya Hifadhi hiyo ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 37 zinaendelea kutumika ikiwemo kuongeza eneo la uwanja, kuendelea kukamilisha majengo ya abiria, kujenga mageti mapya na nyumba za kulala za kisasa.
