Mshambuliaji wa Yanga SC Clement Mzize ametwaa tuzo ya Goli Bora la Mwaka katika CAF Awards 2025.
Goli hilo, alilolifunga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya TP Mazembe, limempa heshima hiyo kubwa katika hafla ya utoaji wa tuzo iliofanyika Morocco. Kutokana na sababu za kiafya, Mzize hakuweza kusafiri na hivyo aliwakilishwa na Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu, jopo la madaktari lilimshauri Mzize kuepuka kutembea umbali mrefu kutokana na upasuaji aliofanyiwa hivi karibuni. Hivyo, tuzo hiyo muhimu ya CAF Awards 2025 imerejea moja kwa moja nyumbani Tanzania.
Katika tuzo hizo, Fiston Mayele, aliyewahi kuihudumia Yanga SC, pia aling’ara baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Mashindano ya Vilabu Barani Afrika (Men’s Interclub Player of the Year).