Kampuni ya huduma za usafiri kupitia mtandao, Bolt, imejizolea tuzo mbili za heshima katika ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kutwaa Tuzo ya Superbrand nchini Kenya na Tuzo ya Huduma Bora za Usafiri wa Kidijitali kwa Mwaka 2026 (Best Digital Mobility Solution of the Year) nchini Tanzania.
Tuzo hizo zinaakisi ukuaji wa kampuni hiyo na mchango wake katika kuimarisha sekta ya usafiri kwa kutumia teknolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Nchini Kenya, Bolt ilitunukiwa Tuzo ya Superbrand katika hafla iliyofanyika jijini Nairobi wiki iliyopita, huku Tanzania ikijinyakulia tuzo yake katika hafla ya Best Brand Awards Africa 2026, ikiwa ni kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kupanua upatikanaji wa huduma za usafiri kupitia teknolojia.
Kwa sasa, Bolt inatoa huduma katika miji na maeneo zaidi ya 10 nchini Tanzania, ikiwezesha mamia ya maelfu ya safari kila siku kupitia magari, pikipiki na bajaji, sambamba na huduma za usafirishaji wa bidhaa na usafiri kwa taasisi na kampuni mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo nchini Tanzania, Meneja Mkuu wa Bolt Afrika Mashariki, **Dimmy Kanyankole**, alisema mafanikio hayo yametokana na imani na ushirikiano wa wateja, madereva na wadau mbalimbali.
“Zaidi ya kubadilisha namna watu wanavyosafiri, tumechangia kufungua fursa za kiuchumi kwa maelfu ya madereva, huku madereva wetu wenye mapato ya juu zaidi wakiwa katika kundi la asilimia 10 ya watu wenye kipato cha juu zaidi nchini.
Aliongeza pia kuwa tuzo hio ni ya Watanzania mamilioni wanaotumia huduma za Bolt, madereva washirika, wadau na wafanyakazi wote waliochangia mafanikio ya kampuni.