Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi ashauri kikundi cha Paza Sauti cha WAVIU kutumia mitandao ya kijamii kutangaza na kuuza bidhaa zao ili kuweza kufikia wateja wengi Zaidi huku akiwapongeza kwajuhudi na umoja wao katika shughuli zao za uzalishaji.
Ametoa ushauri huo alipotembelea kikundi cha Paza Sauti cha wajasiliamali wanaoishi na VVU katika ziara yake ya ufatiliaji utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI katika Wilaya ya Nyamagana, Jijini Mwanza.
“nikiingia kwenye simu yangu sioni kikundi cha Paza Sauti msibanwe na soko la machoni nendeni duniani kupitia mitandao ya kijamii, anzisheni accont ya Instagram muweze kuwafikia hata watu walipo nchi za nje”
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Adam Mrisho alisisitiza kuwa TACAIDS itaendelea kuwekeza katika uwezeshaji wa vijana kiuchumi kama sehemu ya juhudi za kuwaondoa katika mazingira ya changamoto na vishawishi vinavyoweza kuongeza hatari ya maambukizi mapya ya VVU.
“hongereni kwa juhudi na kazi mnazozifanya, hili ni eneo ambalo Tume tumezingatia sana ili kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi”
Vilevile, Dkt. Yonazi alitembelea Kikundi cha Peace and Love kinachojishughulisha na kilimo cha nyanya na matikiti, kinachosimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia Mradi wa DREAMS, unaoratibiwa na TACAIDS kwa kushirikiana na ICAP, Mradi huo unalenga kuwawezesha wanawake na vijana balehe kiuchumi na kijamii ili kupunguza vishawishi vinavyoweza kupelekea maambukizi mapya kwa kundi hili.
Nae, Katibu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Maambukizi Wilaya ya Nyamagana Joseph Kiharate ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuwezesha WAVIU kupata dawa katika hospitali zote na huduma zinatolewa kila siku katika juma.
“tunashukuru tunapata dawa katika hospital izote na huduma zinatolewa siku saba za wiki kupitia nyie afya zetu zinaimarika”
Hata hivyo, Pongezi zimetolewa kwa Jiji la Mwanza kwa kuweza kufanikiwa kufikia lengo la kitaifa la 95-95-95 kwa kiwango cha juu na kuongeza ushirikiano na wadau wakiwemo viongozi wa dini katika mwitikio wa VVU na UKIMWI nchini.
